HESLB Yatangaza Orodha ya Wanufaika 2025/2026

HESLB Yatangaza Orodha ya Wanufaika 2025/2026, Majina ya waliopata Mkopo 2025-2026 – HESLB Loan Beneficiary.

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo, Ijumaa Oktoba 03 2025, imehitimisha kikao kazi cha siku mbili kilichowakutanisha Menejimenti ya HESLB na Maafisa Mikopo kutoka vyuo vya elimu ya juu na vya kati nchini, kilichofanyika katika ukumbi wa Royal Tughimbe jijini Mbeya/HESLB Yatangaza Orodha ya Wanufaika 2025/2026.

Akizungumza wakati wa kufunga kikao hicho kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Mkurugenzi wa Urejeshaji na Urejeshwa Mikopo, CPA(T) George Mziray, alisema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuwekeza katika elimu ya juu kwa kutenga shilingi bilioni 916.5 kwa mwaka wa masomo 2025/2026, fedha zitakazonufaisha zaidi ya wanafunzi 252,000 nchini.

HESLB Yatangaza Orodha ya Wanufaika 2025/2026

HESLB Yatangaza Orodha ya Wanufaika 2025/2026
HESLB Yatangaza Orodha ya Wanufaika 2025/2026

Orodha iliyotangazwa leo inajumuisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliodahiliwa katika vyuo mbalimbali vya elimu ya juu na vyuo vya kati waliopangiwa mikopo kwa ajili ya Shahada ya awali (30,311) yenye thamani ya TZS 93.7 bilioni. Orodha ya awamu ya pili inafanya idadi ya jumla ya wanafunzi 51,645 waliopangiwa mikopo katika awamu ya kwanza na awamu ya pili kwa ajili ya kugharimia masomo yao ya shahada ya awali ikiwa na thamani ya TZS 163.8 bilioni. Kati ya wanafunzi hao, wanafunzi wa kike ni 22,216 (sawa na 43%) na wa kiume 29,429 (sawa na 57%)

Awamu hii ya pii inajumuisha pia mikopo ya Stashahada (Diploma) kwa wanafunzi wapatao 2,157 yenye thamani ya TZS 5.6 bilioni. Wanafunzi wengine 45 ni wa shahada ya uzamili waliopangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 205.6 milioni na wanufaika 16 wa Shahada ya Uzamivu waliopangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 215.6 milioni.

CHECK ALSO: