Hizi hapa Nafasi za Kazi kutoka Jeshi la Uhamiaji | Nafasi za Kazi za Jeshi la Uhamiaji 2024/2025 | Jeshi la Uhamiaji Ajira Mpya pia unaweza kupakua PDF Kwa Maelezo yote. Maelekezo yote kuhusu vigezo na mafunzo kiujumla kupitia tangazo hili la ajira za uhamiaji 2024.
Hizi hapa Nafasi za Kazi kutoka Jeshi la Uhamiaji
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji kwa Mamlaka niliyonayo chini ya Kanuni Namba 11(1) ya Kanuni za Uendeshaji za Uhamiaji za Mwaka 2018, natangaza nafasi za Ajira Mpya za Askari wa Uhamiaji kwa Vijana wa Kitanzania wenye sifa zifuatazo:-
SIFA ZA MWOMBAJI
- Awe ni raia wa Tanzania;
- Awe hana ajira au hajawahi kuajiriwa na Taasisi yoyote Serikalini;
- Awe na Cheti cha Kuzaliwa;
- Awe na Kitambulisho cha Taifa au Namba ya Utambulisho iliyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA);
- Awe na siha njema ya mwili na
- Awe hajawahi kutumia Dawa za kulevya;
- Asiwe na Kumbukumbu au Taarifa zozote za kuhusika katika masuala au matukio ya uhalifu au jinai;
- Asiwe na alama yoyote au michoro (Tatoo) katika mwili wake;
- Awe hajaoa au kuolewa wala kuwa na mtoto;
- Mwombaji mwenye Elimu ya Kidato cha Nne awe na umri kuanzia miaka 18 hadi miaka 22, Mwombaji mwenye Elimu ya Kidato cha Sita na Stashahada awe na umri kuanzia miaka 18 hadi miaka 25 na Mwombaji mwenye Elimu ya Shahada/Stashahada ya Juu awe na umri kuanzia miaka 18 hadi miaka 30.
- Awe tayari kufanya kazi za Idara ya Uhamiaji mahali popote
- Awe tayari kujigharimia katika hatua zote za ufuatiliaji na uendeshwaji wa zoezi la
MAOMBI YATAKAYOPEWA KIPAUMBELE:
Maombi yatakayopewa kipaumbele ni ya waombaji wenye taaluma ngazi ya Shahada/Stashahada ya Juu, Stashahada na Astashahada kutoka katika Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali wenye fani zifuatazo:-
Mtaalamu wa Lugha za Kimataifa, Utawala, Sheria, Uhusiano, TEHAMA, Masijala, Ukatibu Mahsusi, Uhasibu, Ununuzi na Ugavi waliosajiliwa na Bodi, Takwimu, Uchumi, Umeme, Ufundi wa Magari, Ufundi wa AC, Cyber Security, Brass band, na Mpiga chapa (Printer). Hizi hapa Nafasi za Kazi kutoka Jeshi la Uhamiaji
NAMNA YA KUFANYA MAOMBI:
MAOMBI yote ya Ajira yatawasilishwa kupitia tovuti ya Idara ya Uhamiaji ambayo ni https://www.immigration.go.tz kuanzia tarehe 29 Novemba, 2024 na mwisho wa kufanya maombi ni tarehe 13 Disemba, 2024/Hizi hapa Nafasi za Kazi kutoka Jeshi la Uhamiaji.
Wakati wa kufanya Maombi, Mwombaji anatakiwa kuambatisha (upload) kwenye mfumo wa Ajira nyaraka zifuatazo zilizo katika mfumo wa PDF (kila Nyaraka moja isizidi 300Kb);
- Picha (passport size) ya hivi karibuni iliyo katika mfumo wa jpg/png isiyozidi
300Kb kwa ajili ya kuambatisha kwenye mfumo (upload);
- Barua ya maombi ya ajira iliyoandikwa kwa mkono;
- Barua ya Utambulisho toka Serikali ya Mtaa/Kijiji au Shehia; kwa walio Makambini JKT/JKU wawe na barua za Utambulisho kutoka kwa Mkuu wa Kambi;
- Cheti cha Kuzaliwa;
- Awe na Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au Namba ya NIDA kwa ajili ya kujisajili kwenye mfumo;
- Awe na Index namba za vyeti vya kufaulu Kidato cha Nne na Kidato cha Sita ambazo atajaza kwenye mfumo wa ajira;
- Vyeti vingine vya kuhitimu fani mbalimbali ngazi ya Astashahada, Stashahada, na Shahada/Stashahada ya Juu (kama anavyo na viwe vimehakikiwa katika vyuo husika);
- Vyeti vya usajili wa taaluma kwa fani zinazohitaji usajili wa Bodi;
- Wasifu wa Mwombaji (CV).
TAHADHARI
- Maombi yote yatapokelewa katika utaratibu ulioainishwa katika kifungu Namba 3 hapo juu na si vinginevyo;
- Mwombaji yoyote atakayebainika kuwasilisha nyaraka za kughushi atachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa Mahakamani;
- Epuka Matapeli wanaoomba fedha au rushwa ya aina yoyote kwa ajili ya kusaidia kupata nafasi za kazi.
ANGALIA PIA:
Weka maoni yako