Je Pacome au Ahoua Nani Anastahili MVP wa Ligi Kuu NBC 2024/2025? Mjadala kuhusu nani anastahili kuwa MVP wa Ligi Kuu ya NBC kwa msimu wa 2024/2025 umezidi. Aliyekuwa msemaji wa Yanga, Haji Manara amezidisha mjadala kwa kuweka wazi kuwa Zouzoa Pacome ndiye anastahili kutwaa tuzo hiyo msimu huu.
Hata hivyo, mjadala huo umeongezeka zaidi baada ya wahusika kadhaa kutaja Jean Charles Ahoua kama mmoja wa wagombea wanaostahili kuwania tuzo hiyo.
Je Pacome au Ahoua Nani Anastahili MVP wa Ligi Kuu NBC 2024/2025?
Takwimu za Msimu Huu (Hadi Sasa):

Jean Charles Ahoua: Magoli 16 | Assist 09
Zouzoa Pacome: Magoli 11 | Assist 08
Kwa kuzingatia takwimu pekee, Ahoua anaonekana kutangulia mbele kidogo. Lakini je, MVP hupimwa kwa magoli tu?

Wachezaji Wanaostahili Kugombea MVP 2024/2025:
Kwa mujibu wa mjadala unaoendelea, hawa ni wachezaji wanaoonekana kuwa na nafasi kubwa ya kugombea tuzo ya MVP ya NBC Premier League 2024/2025:
- Zouzoa Pacome
- Jean Charles Ahoua
- Feisal Salum
- Dickson Job
- Clement Mzize
Kwa mujibu wa vigezo vya kitaalamu vya kuchagua MVP, ni hoja zuri ya kumtaja Pacome kwenye kinyanganyiro. Hata hivyo, hoja za wanaomtaja Ahoua hazipaswi kuchukuliwa kirahisi, hasa kwa kuzingatia ubora wa takwimu zake za kibinafsi. Tuzo hii inahitaji uchambuzi wa kina, sio tu wa takwimu, lakini pia mchango wa jumla wa mchezaji, ufanisi na thamani kwa timu yake.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako