Jean Ahoua Arejea Simba SC Kujiandaa na Msimu Mpya

Jean Ahoua Arejea Simba SC Kujiandaa na Msimu Mpya: Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya NBC msimu uliopita, Jean Ahoua, amerejea rasmi jijini Dar es Salaam leo baada ya likizo yake tayari kujiunga na kikosi cha Simba SC na kuanza mazoezi kwa ajili ya msimu mpya wa 2025/2026.

Jean Ahoua Arejea Simba SC Kujiandaa na Msimu Mpya

Ahoua ambaye aling’ara kama kiungo mkabaji msimu uliopita, anatarajiwa kuwa mmoja wa wachezaji wakongwe watakaochangia kwa kiasi kikubwa katika kampeni za Simba SC ndani na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Jean Ahoua Arejea Simba SC Kujiandaa na Msimu Mpya

Licha ya kipaji chake, taarifa zinaeleza kuwa tayari klabu kadhaa nje ya Tanzania zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili Jean Ahoua. Hata hivyo, hadi sasa hakuna ofa rasmi iliyowasilishwa kwa bodi ya Simba SC.

“Tuna taarifa kwamba kuna vilabu vinavutiwa naye, lakini hakuna ofa rasmi iliyokuja. Yupo hapa tayari kujiunga na maandalizi ya msimu mpya.”

CHECK ALSO:

  1. Utajiri Wa Cristiano Ronaldo Wafika Bilioni Dola za Marekani
  2. CV ya Neo Maema Mchezaji Mpya wa Simba SC 2025/2026
  3. Jonathan Sowah Ajiunga na Simba SC Kutoka Singida Black Stars
  4. Abdulhamid Moalin Aondoka Yanga SC, Ajiunga na CR Belouizdad ya Algeria