Jezi Mpya za Simba 2025 Zavujishwa Mitandaoni

Jezi Mpya za Simba 2025 Zavujishwa Mitandaoni, Mashabiki Wahoji Usiri wa Klabu: Taarifa za kuvuja kwa picha za jezi mpya za Simba SC zimezua mjadala mkubwa kwa mashabiki wa soka nchini. Mitandaoni picha hizo zimeanza kutolewa na baadhi ya mashabiki wa Yanga pamoja na mwanahabari İbrahim Ambokile zikizua hisia tofauti.

Mashabiki wengi wa Simba wameeleza kuwa jezi hizo zikithibitishwa kuwa rasmi zina ubora wa hali ya juu na zinaonekana kuvutia zaidi ya zile zilizotolewa awali. Baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo wameapa kununua jezi hizo za rangi zote mara tu zitakapozinduliwa rasmi.

Jezi Mpya za Simba 2025 Zavujishwa Mitandaoni

Licha ya sifa za kuonekana kwa jezi hiyo, utata mkubwa uliotawala mijadala hiyo ulihusu uvujaji wa siri ndani ya Simba SC. Mashabiki wanajiuliza ni nani anahusika kutoa taarifa za upendeleo na kwa nini klabu haijamtambua mtu huyo.

Kwa maoni ya wengi, tatizo la uvujaji wa siri limekuwa likiichafua Simba, hasa katika mechi muhimu dhidi ya wapinzani wake wa jadi, Yanga SC. Mashabiki wanahofia hali hii inaweza kuathiri morali ya wachezaji wapya, pia kuipa klabu changamoto kubwa ya kuchuana na timu zilizoimarika zaidi msimu huu, ambazo ni Azam FC na Singida Black Stars.

Jezi Mpya za Simba 2025 Zavujishwa Mitandaoni
Jezi Mpya za Simba 2025 Zavujishwa Mitandaoni

Simba SC inatarajiwa kuzindua rasmi jezi zake mpya tarehe 30, itakapofahamika iwapo picha zilizovuja mtandaoni zinaendana na jezi halisi. Wakati huo huo, mashabiki wanautaka uongozi wa klabu hiyo kuimarisha usiri na kuwachukulia hatua waliohusika kutoa taarifa ili kulinda heshima ya klabu.

Jezi mpya za Simba SC tayari zimevutia mashabiki wengi, lakini mjadala mkubwa unaendelea kuhusu kuvuja kwa siri za ndani ya klabu. Mashabiki wanautaka uongozi kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha klabu inaimarika ndani na nje ya uwanja.

SOMA PIA:

  1. Ngao ya Jamii 2025 Simba SC vs Yanga SC Septemba 16 Benjamin Mkapa
  2. Flambeau Du Centre na Aigle Noir CS Zajiondoa CECAFA Kagame Cup 2025
  3. Simba Kuwaaga Wachezaji wa Zamani Bocco na Mkude
  4. Viingilio Simba Day 2025, Bei za Tiketi na Maelekezo Muhimu kwa Mashabiki