Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Darasa la Saba 2025, Hatua Kamili za Kukagua Matokeo ya PSLE kwa Urahisi Kupitia NECTA.
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza rasmi matokeo ya Cheti cha Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) kwa mwaka 2025. Matokeo haya ni muhimu kwa wanafunzi waliomaliza mwaka wa 7 mwaka huu, kwa kuwa ndiyo huamua maendeleo yao kuelekea elimu ya sekondari.
Kwa mujibu wa taarifa ya NECTA, matokeo haya yanapatikana rasmi kwenye tovuti ya baraza hilo na yanaweza kufikiwa na wanafunzi wote kwa kutumia simu au kompyuta.
Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Darasa la Saba 2025
Hatua za Kuangalia Matokeo Kupitia Tovuti ya NECTA
Fuata hatua zifuatazo ili kuangalia matokeo yako ya Darasa la Saba 2025:
-
Tembelea Tovuti ya NECTA
Fungua kivinjari (browser) kwenye simu au kompyuta yako, kisha nenda kwenye tovuti rasmi ya NECTA:
👉 www.necta.go.tz -
Fungua Sehemu ya Matokeo (Results)
Baada ya kufika kwenye ukurasa wa mwanzo, tafuta kipengele kilichoandikwa “Matokeo” au “Results”, kisha bofya “PSLE 2025” (Matokeo ya Darasa la Saba 2025). -
Chagua Mkoa na Wilaya
Orodha ya mikoa yote ya Tanzania itaonekana. Bonyeza jina la mkoa unaotoka, kisha chagua wilaya yako. -
Tafuta Shule Yako
Baada ya kuchagua wilaya, utaona orodha ya shule zote. Tafuta na bonyeza jina la shule yako kuona matokeo. -
Angalia Matokeo
Ukurasa wa shule yako utafunguka ukiwa na majina ya wanafunzi na alama zao kwa kila somo. Tafuta jina lako au namba ya mtihani ili kuona matokeo yako binafsi. -
Pakua au Chapisha Matokeo
Unaweza kupakua (download) au kuchapisha matokeo yako moja kwa moja kutoka kwenye tovuti ya NECTA kwa matumizi ya baadaye.

👉 Angalia Matokeo Moja kwa Moja Hapa:
🔗 Results | NECTA
NECTA wakati mwingine hutoa huduma ya kuangalia matokeo kupitia ujumbe mfupi (SMS). Hata hivyo, huduma hii inapatikana tu wakati tangazo rasmi linafanywa. Hivi sasa, njia salama na ya kuaminika ni kupitia tovuti rasmi ya NECTA.
Tafsiri ya Alama na Madaraja ya Ufaulu
Katika matokeo ya PSLE, kila mwanafunzi hupata alama katika kila somo. Alama hizi huamua daraja la ufaulu kama ifuatavyo:
Herufi | Maelezo ya Ufaulu |
---|---|
A | Ufaulu wa juu sana |
B | Ufaulu wa juu |
C | Ufaulu wa kati |
D | Ufaulu wa chini |
F | Hajafaulu |
Wanafunzi wanaopata madaraja ya juu (A, B, au C) huwa na nafasi kubwa ya kuchaguliwa kujiunga na shule bora za sekondari kupitia mfumo wa uchaguzi wa kitaifa unaoratibiwa na TAMISEMI.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako