JINSI YA KULIPIA ADA YA UANACHAMA YANGA SC: Yanga SC Yazindua Kampeni ya “Tofali la Ubingwa” – Wanachama Wahimizwa Kulipia Ada Kupitia M-Pesa, Airtel Money na Mixx.
Young Africans SC (Yanga SC) imezindua rasmi kampeni kabambe ya “Timu ya Ubingwa”, yenye kauli mbiu “Tunajijenga,” ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kujenga klabu imara kwa ajili ya msimu wa 2025/26.
Kupitia kampeni hii wanachama wote wa Yanga SC wanahamasishwa kulipa ada zao za uanachama, huku mashabiki wapya wakialikwa kujiunga rasmi na klabu hiyo. Lengo kuu la kampeni hiyo ni kufikia wanachama milioni moja, jambo ambalo litaiwezesha klabu kupata uhuru wa kifedha na usimamizi bora wa shughuli zake.
JINSI YA KULIPIA ADA YA UANACHAMA YANGA SC
Kampeni hii inaungwa mkono na SportPesa, ambaye ni mdhamini mkuu wa klabu. Pia inabeba uzito mkubwa kiutawala, kwani inalenga kuimarisha ushirikishwaji wa wanachama katika maendeleo ya klabu yao.

JINSI YA KULIPIA ADA YA UANACHAMA KUPITIA M-PESA (Vodacom):
-
Piga *150*00#
-
Chagua 4 – LIPA KWA M-PESA
-
Chagua 4 – Weka Namba ya Kampuni
-
Ingiza Namba ya Kampuni: 888844
-
Weka Namba ya Kumbukumbu (weka namba yako ya simu)
-
Weka kiasi:
-
24,000 TZS kwa mwaka mmoja
-
48,000 TZS kwa miaka miwili
-
-
Weka namba yako ya siri
-
Ingiza 1 kukubali
NAMBA ZA MALIPO KWA MITANDAO MINGINE:
-
Airtel Money: Namba ya Kampuni: 555533
-
Mixx by YAS: Namba ya Kampuni: 888844
CHECK ALSO:






Weka maoni yako