Jinsi ya Kutuma Maombi Ajira Jeshi la Polisi 2025

Jinsi ya Kutuma Maombi Ajira Jeshi la Polisi 2025, Nafasi za Polisi 2025 Tangazo la Ajira Jeshi la Polisi | Nafasi za Ajira Jeshi la Polisi Tanzania 2025 Sifa, Tarehe Muhimu na Jinsi ya Kutuma Maombi. Jeshi la Polisi Tanzania limetangaza nafasi za kazi kwa vijana wa kitanzania wenye shahada za kwanza, stashahada, cheti na kidato cha sita na nne.

Nafasi hizi ziko wazi kwa waombaji wenye sifa, kwa mujibu wa tangazo rasmi lililotolewa na Inspekta Jenerali wa Polisi Tanzania (IGP), Camilius Wambura, Machi 20, 2025/Jinsi ya Kutuma Maombi Ajira Jeshi la Polisi 2025.

Jinsi ya Kutuma Maombi Ajira Jeshi la Polisi 2025

Jinsi ya Kutuma Maombi

📌 Mwisho wa kutuma maombi: Aprili 4, 2025

  1. Barua ya maombi iandikwe kwa mkono na iambatishwe katika mfumo wa PDF.
  2. Maombi yafanywe kupitia mfumo rasmi wa Ajira wa Jeshi la Polisi unaopatikana kwenye tovuti/Nafasi za Polisi 2025 Tangazo la Ajira Jeshi la Polisi: https://ajira.tpf.go.tz.
  3. Maombi kupitia barua pepe, posta au kupeleka kwa mkono hayatapokelewa.

Fani Zinazohitajika

Jinsi ya Kutuma Maombi Ajira Jeshi la Polisi 2025
Jinsi ya Kutuma Maombi Ajira Jeshi la Polisi 2025

Kwa waombaji wa shahada, stashahada na astashahada, fani zinazohitajika zinajumuisha:

Tanzania Bara (Shahada)

  • Uhandisi wa Umeme, Uhandisi wa Mitambo, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT)
  • Udaktari wa Binadamu, Uuguzi, Tiba ya Radiolojia
  • Usimamizi wa Ardhi, Sheria, Uchunguzi wa Jinai na Usalama wa Mtandao
  • Sayansi ya Mifugo, Sayansi ya Mazingira, Uandishi wa Habari
  • Lugha za Kigeni: Kifaransa, Kireno, Kichina na Kiarabu

Zanzibar (Shahada)

  • Uhasibu na Fedha, Uhandisi wa Kiraia, Sayansi ya Kompyuta
  • Uandishi wa Habari na Utangazaji, Sheria, Tiba ya Binadamu
  • Uuguzi, Dawa za Binadamu, Ugavi na Manunuzi

Stashahada (Diploma) na Astashahada (Certificate)

  • Udaktari wa Kinywa, Sayansi ya Uchunguzi wa Jinai, Usanifu wa Picha na Video
  • Ufundi wa Magari, Uhandisi wa Umeme, Usanifu wa Majengo
  • Uuguzi na Ukunga, Uendeshaji wa Mitambo, Muziki na Sanaa za Maonyesho
  • Usanifu wa Mavazi, Ushonaji, Ufundi wa Mabomba na Ujenzi

Jeshi la Polisi limeeleza kuwa waombaji lazima wawe tayari kufanya kazi popote nchini na kuhudhuria mafunzo ya taaluma ya polisi. Ajira hizi ni fursa muhimu kwa vijana wa Kitanzania wenye sifa stahiki. Waombaji wanahimizwa kukidhi mahitaji yote na kuwasilisha maombi yao kabla ya tarehe ya mwisho.

CHECK ALSO: