JKT Queens Watwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara 2024/25

JKT Queens Watwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara 2024/25: Klabu ya JKT Queens imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara msimu wa 2024/2025 baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Gets Program katika mchezo wa mwisho wa msimu huu.

JKT Queens Watwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara 2024/25

Ushindi huo umeiwezesha JKT Queens kutwaa taji hilo kwa tofauti ya mabao 20, licha ya kuwa wamefungana pointi na Simba Queens iliyoshika nafasi ya pili.

Kwa matokeo hayo, JKT Queens ilimaliza msimu ikiwa na pointi 47 baada ya mechi 18, sawa na Simba Queens. Hata hivyo, tofauti ya mabao iliipa JKT Queens ubingwa, ikiwa ni mara ya tano katika historia yao kutwaa taji hilo.

JKT Queens Watwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara 2024/25
JKT Queens Watwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara 2024/25

Kwa sasa JKT Queens inaongoza kwa historia ya Ligi Kuu ya Wanawake kwa kutwaa mataji mengi (5), ikifuatiwa na Simba Queens iliyotwaa mara nne.

Yanga Princess walimaliza msimu wakiwa nafasi ya tatu wakiwa na pointi 37, huku Mashujaa Queens wakimaliza nafasi nne za juu wakiwa na pointi 31, zote baada ya mechi 18.

Msimamo wa Mwisho wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara 2024/25 (Top 4):

  1. JKT Queens – Alama 47 (Tofauti ya mabao: +20)

  2. Simba Queens – Alama 47

  3. Yanga Princess – Alama 37

  4. Mashujaa Queens – Alama 31

CHECK ALSO: