JKT Tanzania Yaachana na Wachezaji 7, Dirisha Kubwa La Usajili 2025/26

JKT Tanzania Yaachana na Wachezaji 7, Dirisha Kubwa La Usajili 2025/26: JKT Tanzania Yawaaga Wachezaji 7 Bila Kutangaza Usajili Mpya.

JKT Tanzania yenye maskani yake Mbweni, Dar es Salaam, imeanza kukifanyia marekebisho kikosi chake kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuwaachia wachezaji saba (7). Hadi sasa klabu hiyo haijatangaza rasmi kuongeza wachezaji wapya licha ya tetesi mbalimbali kuhusu usajili huo.

Hatua hii inaashiria mabadiliko ya kimkakati katika kikosi hicho, kwani kikosi cha makocha kinaonekana kuainisha mikakati ya kukisuka upya kikosi hicho ili kuweza kutamba vilivyo msimu wa 2025/2026.

JKT Tanzania Yaachana na Wachezaji 7, Dirisha Kubwa La Usajili 2025/26

Orodha ya Wachezaji Walioachwa na JKT Tanzania:

  1. George Wawa

  2. Matheo Anthony

  3. Ismaily Aziz Kader

  4. Siraji Ramadhan

  5. Sixtus Sabilo

  6. Ismail Nakapi

  7. Martin Kigi

JKT Tanzania Yaachana na Wachezaji 7, Dirisha Kubwa La Usajili 2025/26
JKT Tanzania Yaachana na Wachezaji 7, Dirisha Kubwa La Usajili 2025/26

Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani ya klabu, wachezaji hao wameachwa kwa sababu mbalimbali, zikiwemo sababu za kiufundi na kumalizika kwa mikataba yao. Hata hivyo, hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuhusu ni lini klabu itaanza kutangaza usajili mpya.

Uamuzi wa kuwatoa wachezaji saba unaonyesha nia ya JKT Tanzania kujipanga upya kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu. Mashabiki na wadau wa soka wanasubiri kwa hamu hatua zinazofuata, hasa kuhusu wachezaji wapya waliosajiliwa na maandalizi ya timu kwa ajili ya msimu wa 2025/2026. Klabu hiyo ina nafasi ya kutumia fursa ya soko la usajili kuimarisha kikosi chake na kupata mafanikio makubwa.

CHECK ALSO:

  1. Mashujaa FC Wameachana na Wachezaji 10 Kuelekea Ligi Kuu Bara 2025/2026
  2. Simba SC Yasaini Mkataba wa Udhamini na Betway wa Bilioni 20 kwa Miaka Mitatu
  3. Marcio Maximo Atangazwa Kocha Mpya wa KMC FC 2025
  4. Mohammed Bajaber Asaini Mkataba wa Miaka Miwili na Simba SC