Jonathan Ngwem Ajiunga na Kambi ya Simba Nchini Misri kwa Majaribio

Jonathan Ngwem Ajiunga na Kambi ya Simba Nchini Misri kwa Majaribio: Beki wa kushoto raia wa Cameroon, Jonathan Ngwem ameanza mazoezi rasmi na klabu ya Simba Sports Club ya Tanzania, iliyopo nchini Misri kwa ajili ya msimu wa 2025/2026.

Jonathan Ngwem Ajiunga na Kambi ya Simba Nchini Misri kwa Majaribio

Akiwa mchezaji huru kufuatia kumalizika kwa mkataba wake na klabu ya Modern Future FC ya Misri, Ngwem kwa sasa anafanya mazoezi na Wekundu hao wa Msimbazi kwa ajili ya majaribio ya kutathmini ujuzi wake kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho kuhusu uhamisho wake.

Kwa mujibu wa habari za ndani ya klabu hiyo, kocha wa Simba SC, Fadlu Davids ndiye anayesimamia majaribio ya Jonathan Ngwem. Iwapo itaridhika na utendaji wake, Simba SC itamsainisha mkataba wa mwaka mmoja.

Jonathan Ngwem Ajiunga na Kambi ya Simba Nchini Misri kwa Majaribio
Jonathan Ngwem Ajiunga na Kambi ya Simba Nchini Misri kwa Majaribio

Ngwem mwenye uzoefu wa soka la kimataifa ana uwezo wa kucheza nafasi ya beki wa kushoto na amecheza kwa misimu kadhaa na timu ya taifa ya Cameroon (The Indomitable Lions).

Endapo Ngwem atasajiliwa ataongeza ushindani kwenye nafasi ya beki wa kushoto ambayo tayari imeimarishwa na ujio wa Anthony Mligo kutoka Namungo FC. Simba SC inaendelea kuonyesha dhamira ya dhati ya kufikia msimu bora zaidi ndani na nje ya Tanzania.

CHECK ALSO:

  1. Simba Yamsajili Anthony Mligo Kutoka Namungo FC
  2. Droo ya CAF 2025/26 Kufanyika Azam TV, Agosti 9 Saa 8 Mchana
  3. Ratiba ya CHAN 2025 Leo
  4. Msimamo wa CHAN 2024/2025 Taifa Stars