KARIAKOO DERBY Kocha wa Simba, Fadlu Aeleza Hamasa ya Kikosi

KARIAKOO DERBY Kocha wa Simba, Fadlu Aeleza Hamasa ya Kikosi | Kocha wa Simba SC, Fadlu Davids amesema kuna furaha kubwa ndani ya timu hiyo kuelekea Kariakoo derby dhidi ya Yanga SC. Wachezaji wote wana hamu ya kushiriki katika mechi hiyo muhimu, ambayo inaongeza ushindani wa juu katika mafunzo.

KARIAKOO DERBY Kocha wa Simba, Fadlu Aeleza Hamasa ya Kikosi

Davids pia alifichua kuwa bado wanasubiri kipa Moussa Camara na beki Che Malone Fondoh kufanyiwa tathmini ya mwisho kubaini kama watakuwa tayari kucheza, kulingana na utimamu wao.

Naye nahodha Msaidizi wa Simba, Shomari Kapombe, alisema matokeo ya mechi zilizopita yamewekwa pembeni na sasa akili yao iko kwenye mchezo huu mkubwa kwa watani wa jadi.

KARIAKOO DERBY Kocha wa Simba, Fadlu Aeleza Hamasa ya Kikosi

Mchezo kati ya Simba SC na Yanga SC unatarajiwa kuwa kati ya mchezo mkali na wa kusisimua, huku mashabiki wakisubiri kwa hamu kuona nani ataibuka na ushindi.

ANGALIA PIA: