Kibu Denis Yupo na Klabu ya Kristiansund BK kwa Majaribio Nchini Norway

Kibu Denis Yupo na Klabu ya Kristiansund BK kwa Majaribio Nchini Norway: Imethibitishwa kuwa nyota wa Simba SC na timu ya Taifa ya Tanzania, Kibu Denis anaendelea na majaribio na klabu ya Kristiansund BK inayoshiriki Ligi Kuu ya Norway. Ijapokuwa awali iliripotiwa kuwa alikuwa Marekani kwa mapumziko ya kawaida, lakini taarifa mpya zinasema kuwa mchezaji huyo kwa sasa yuko kwenye mazoezi ya wiki mbili na klabu hiyo ya Norway ili kuona iwapo anaweza kusaini.

Kibu Denis Yupo na Klabu ya Kristiansund BK kwa Majaribio Nchini Norway

Kwa mujibu wa chanzo makini, Kibu ameamua kutumia mapumziko yake ya kujiandaa na msimu mpya nchini Marekani kujiunga na majaribio ya Kristiansund BK, uamuzi anaoufanya kimya kimya bila kutangazwa rasmi hadi makubaliano yatakapofikiwa katika mazungumzo hayo.

“Kibu bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Simba, hivyo ni mchezaji halali wa klabu hiyo. Uongozi wa Simba unafahamu kilichopo,” alisema rafiki wa karibu wa mchezaji huyo.

Kristiansund BK si mgeni kwa Kibu, tayari amefanya majaribio na klabu hiyo kwa msimu wa 2023/2024, ingawa mkataba huo haukuwa rasmi wakati huo. Wakati huu, ana matumaini zaidi anapofanya mazoezi na timu, akilenga nafasi rasmi ya kujiunga/Kibu Denis Yupo na Klabu ya Kristiansund BK kwa Majaribio Nchini Norway.

Kibu Denis Yupo na Klabu ya Kristiansund BK kwa Majaribio Nchini Norway
Kibu Denis Yupo na Klabu ya Kristiansund BK kwa Majaribio Nchini Norway

Taifa Stars Inaendelea Bila Kibu

Wakati Kibu akiendelea na majaribio nchini Norway, Kocha wa Taifa Stars, Hemed Suleiman ‘Morocco’ amechukua hatua ya kuziba nafasi yake kwenye kikosi kinachojiandaa na michuano ya CHAN 2024. Taifa Stars kwa sasa ipo katika kambi ya maandalizi ya michuano hiyo mikubwa ya ndani ya nchi itakayoanza Agosti 2 hadi 30 katika nchi shiriki za Afrika Mashariki za Tanzania, Kenya na Uganda.

Kibu alitarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Taifa Stars kilichopangwa kuelekea nchini Misri kwa ajili ya kambi maalum ya mazoezi, lakini kukosekana kwake kumehusishwa moja kwa moja na kupata nafasi ya kuimarisha soka lake barani Ulaya kwa majaribio.

Hali ya Mkataba wa Simba SC

Kibu Denis amesalia kuwa mchezaji halali wa Simba SC, akiwa amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake. Endapo vipimo hivi vitafanikiwa taratibu za usajili zitakamilika kwa kufuata taratibu za kisheria kati ya Kristiansund BK na Simba SC.

Kwa mujibu wa kanuni za soka za kimataifa, mchezaji aliye na mkataba hawezi kuingia makubaliano na klabu nyingine bila ridhaa ya klabu yake ya sasa. Kwa hiyo uhamisho ukipangwa lazima Simba SC iwe sehemu ya makubaliano hayo/Kibu Denis Yupo na Klabu ya Kristiansund BK kwa Majaribio Nchini Norway.

CHECK ALSO:

  1. Waamuzi Watanzania Arajiga na Ally Hamdani Wateuliwa Kwa CHAN 2024/2025
  2. KIKOSI Cha DR Congo cha CHAN 2025
  3. KIKOSI Cha Burkina Faso cha CHAN 2025
  4. Maandalizi ya CHAN Tanzania, Kenya, Uganda na Congo Brazzaville Kujipima