Kikosi cha Simba dhidi ya Coastal Union Leo 01/03/2025, Matokeo ya Coastal Union vs Simba SC Leo 01/03/2025 | Simba SC vs Coastal Union Leo: Dakika 90 za maamuzi kabla ya Kariakoo derby.
Simba SC wapo jijini Arusha kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union, utakaopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Hii ni mechi muhimu kwa Wekundu hao wa Msimbazi ambao wapo kwenye mbio za kuwania ubingwa wa ligi hiyo msimu huu.
Mechi hii ina umuhimu mkubwa kwa Simba SC kwani matokeo yake yatatoa mwelekeo wa hali yao kuelekea mchezo wa Kariakoo derby dhidi ya Yanga SC, unaotarajiwa kupigwa wikiendi ijayo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa. Kocha wa Simba anatarajiwa kutumia mechi hii kuhakikisha timu yake inaimarika na kupata matokeo mazuri kabla ya mtihani huo mgumu kwa watani wao wa jadi.
Coastal Union si timu ya kuichezea hasa inapocheza nyumbani mbele ya mashabiki wao. Wanajua umuhimu wa mechi hii na watajaribu kutumia faida ya nyumbani kuwazuia Simba SC. Hii inaifanya mechi hii kuwa na mchuano mkali kwa timu zote mbili, huku Coastal Union ikitaka kuvuna pointi muhimu ili kuboresha msimamo wao wa ligi.
Kikosi cha Simba dhidi ya Coastal Union Leo 01/03/2025
Hiki hapa kikosi cah Simba kinachoanza leo kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union kwenye NBC Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025
- Ally Katoro
- Kapombe
- Zimbwe JR
- Chamou
- Spear JR
- Ngoma
- Kagoma
- Ahoua
- Mpanzu
- Ateba
- Kibu

CHECK ALSO:
Weka maoni yako