KIKOSI cha Simba Leo Vs Al Zulfi 20/08/2025 Pre Season: Simba SC vs Al Zulfi Leo Saa 11:30 Jioni | Mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki Saudi Arabia.
Klabu ya Simba SC ya Tanzania inatarajiwa kushuka dimbani leo saa 11:30 Jioni kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Al Zulfi FC ya Saudi Arabia. Mechi hii ni sehemu ya maandalizi ya timu kwa ajili ya msimu mpya wa mashindano ya ndani na nje ya nchi.
Simba SC imekuwa ikitumia fursa ya mechi za kirafiki nje ya nchi kuongeza uzoefu wa wachezaji wake na kuimarisha muunganiko wa kikosi kipya kwa ajili ya msimu ujao. Mechi dhidi ya Al Zulfi inatarajiwa kutoa nafasi kwa wakufunzi hao kuwapima ujuzi wachezaji wapya na wakongwe, pamoja na kujaribu mbinu mbalimbali za kiufundi.
Kwa Al Zulfi, hii ni mechi ya heshima na majaribio, huku wakichukua fursa hiyo kuonyesha ujuzi wao dhidi ya moja ya klabu kubwa barani Afrika.

KIKOSI cha Simba Leo Vs Al Zulfi 20/08/2025
Kikosi cha Simba kinachoaza leo kwenye mchezo dhidi ya Al Zulfi ya Saudi Arabia
1. Camara 🇬🇳
2. Chasambi 🇹🇿
3. Naby Camara 🇬🇳
4. Mbegu 🇹🇿
5. Chamou 🇨🇮
6. Semfuko 🇹🇿
7. Mpanzu 🇨🇩
8. Morice Abraham 🇹🇿
9. Sowah 🇬ðŸ‡
10. Ahoua 🇨🇮
11. Kibu Denis 🇹🇿
SOMA PIA:
Weka maoni yako