KIKOSI cha Simba Leo vs RS Berkane CAF 25/05/2025 | Simba SC vs RS Berkane Fainali Kombe la Shirikisho CAF Mkondo wa Pili.
Simba SC ya Tanzania inatarajiwa kushuka dimbani Jumapili kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa pili wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane ya Morocco. Mchezo huu wa kihistoria utapigwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar, kuanzia saa 10:00 jioni. Saa za Afrika Mashariki.
Katika mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Morocco, Simba SC ilipokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa wenyeji RS Berkane. Hii ina maana Simba inakabiliwa na kibarua kigumu cha kupindua matokeo ili kutwaa kombe hilo kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo.
KIKOSI cha Simba Leo vs RS Berkane CAF 25/05/2025
Kikosi kinachoanza kwenye mchezo wa Simba dhidi ya RS Berkane:-

- CAMARRA
- KAPOMBE
- ZIMBWE JR
- CHAMOU
- CHE MALONE
- NGOMA
- KAGOMA
- MPANZU
- AHOUA
- MUKWALA
- MUTALE
Simba SC inalazimika kuonyesha kiwango cha juu na nidhamu ya hali ya juu katika safu zote, hususan ulinzi na ushambuliaji. Kucheza mbele ya mashabiki wa nyumbani katika uwanja wa Amaan kunatarajiwa kuwa chachu ya motisha kwa wachezaji wa Simba.
Kocha wa Simba SC atategemea wachezaji wake nyota kama Ellie Mpanzu, Jean Ahoua, na Kibu Denis kuiongoza timu kwenye safari ya kuandika historia mpya ya soka la Tanzania.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako