KIKOSI cha Simba Leo Vs Wadi Degla 26/08/2025: Leo Agosti 26, 2025 Simba Sports Club inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Wadi Degla ya Misri. Mechi hiyo itachezwa saa 11:o0 jioni kwa saa za Afrika Mashariki, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu mpya wa 2025/26.
Mechi hii ni sehemu ya ziara ya Simba SC ya kujiandaa na msimu mpya nchini Misri, lengo kuu ikiwa ni kuimarisha ujuzi wa kiufundi, kuboresha uelewa wa wachezaji, na kuwapa uzoefu wa kimataifa kabla ya kuingia kwenye michuano muhimu kama vile Ligi Kuu ya NBC Tanzania na Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League).
Kwa upande wa mpinzani wao, Wadi Degla ni timu inayoshiriki Ligi Kuu ya Misri. Hadi sasa msimu huu, wamecheza mechi nne, wakivuna jumla ya pointi nne baada ya kushinda moja na kutoka sare moja. Katika mechi yao ya mwisho, iliyochezwa jana, Wadi Degla iliishinda ZED 2-1.
KIKOSI cha Simba Leo Vs Wadi Degla 26/08/2025

Kwa Simba SC, hii ni fursa ya kwanza ya kupima ujuzi wa timu hiyo baada ya wiki kadhaa za maandalizi. Zaidi ya hayo, mashabiki wanatumai nyota wapya waliojiunga na timu hiyo watapata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao.
Mchezo wa leo kati ya Simba SC na Wadi Degla unatarajiwa kuwa mtihani kwa Wekundu hao wa Msimbazi kuelekea msimu mpya. Ushindi au sare haitakuwa sababu pekee ya kuamua; ujuzi wa wachezaji na mbinu mpya zitazingatiwa katika kuamua mafanikio ya ziara hii ya maandalizi.
SOMA PIA:
Weka maoni yako