Kikosi cha Taifa Stars Kwenye Mashindano ya CHAN 2024/2025 | Kikosi Rasmi cha Taifa Stars kwa CHAN 2024 | Kambi Kuanza Julai 7, 2025, nchini Misri
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kikosi rasmi cha timu ya Taifa (Taifa Stars) kitakachoanza kambi Julai 7, 2025 nchini Misri kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) 2024. Michuano ya CHAN inatarajiwa kufanyika kwa pamoja katika nchi tatu za Afrika Mashariki: Kenya, Tanzania na Uganda.
Kikosi hicho kilichotangazwa na kocha Hemed Suleiman kinajumuisha wachezaji kutoka klabu kadhaa za Tanzania, zikiwemo Simba SC, Young Africans, Azam FC, Coastal Union, Singida Big Stars, JKT Tanzania, na timu ya vijana Ngorongoro Heroes.
Kikosi cha Taifa Stars Kwenye Mashindano ya CHAN 2024/2025

Orodha Kamili ya Wachezaji Walioitwa:
Walinda Mlango:
Aishi Manula (Simba SC)
Hussein Masalanga (Singida BS)
Yakoub Suleiman (JKT Tanzania)Mabeki:
Shomari Kapombe (Simba SC)
Lusajo Mwaikenda (Azam FC)
Mohamed Hussein (Simba SC)
Paschal Msindo (Azam FC)
Dickson Job (Young Africans)
Wilson Nangu (JKT Tanzania)
Abdulrazack Mohamed (Simba SC)
Vedastus Masinde (U20 Ngorongoro Heroes / TMA)
Lameck Lawi (Coastal Union)Viungo:
Ibrahim Hamad (Young Africans)
Ahmed Pipino (U20 Ngorongoro Heroes / KMC)
Mudathir Yahya (Young Africans)
Yusuph Kagoma (Simba SC)
Nassor Saadun (Azam FC)
Jammy Simba (U20 Ngorongoro Heroes / KMC)
Iddy Selemani (Azam FC)
Sabry Kondo (Coastal Union)
Feisal Salum (Azam FC)
Sheikhan Khamis (U20 Ngorongoro Heroes / Young Africans)
Clement Mzize (Young Africans)
Mishano Michael (U20 Ngorongoro Heroes / Kengold FC)Washambuliaji:
Kibu Denis (Simba SC)
Ibrahim Hamad (Tabora United)
Abdul Suleiman (Azam FC)
Wachezaji hawa wataingia kambini nchini Misri kwa maandalizi ya mwisho kabla ya michuano hiyo kuanza. CHAN 2024 inawapa wachezaji kutoka ligi za ndani fursa ya kuonyesha vipaji vyao katika ngazi ya kimataifa/Kikosi cha Taifa Stars Kwenye Mashindano ya CHAN 2024/2025.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako