KIKOSI Cha Taifa Stars Leo vs Burkina Faso 02/08/2025: CHAN 2024 Yaanza Rasmi Leo, Tanzania Kuikabili Burkina Faso Katika Mchezo wa Ufunguzi.
Michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) 2024 inafunguliwa rasmi leo Agosti 2, 2025. Tanzania ikiwa mwenyeji wa michuano hiyo itamenyana na Burkina Faso katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi.
Mechi hii ya ufunguzi itachezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, ikiwa ni mwanzo wa mbio za kihistoria kwa Taifa Stars katika mashindano hayo muhimu kwa wachezaji wa ligi za ndani.
Watanzania wengi wamekuwa wakiisubiri kwa hamu siku hii, wakitarajia kuona soka la hali ya juu na mafanikio kwa timu ya taifa nchini mwao. Serikali na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wamewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao na kuwapa motisha wachezaji.
KIKOSI Cha Taifa Stars Leo vs Burkina Faso 02/08/2025
KIKOSI CHA TANZANIA

- YAKOUB
- ZIMBWE
- BACCA
- JOB
- KAPOMBE
- MUDATHIRU
- KAGOMA
- IDDI
- FEI TOTO
- SOPU
- MZIZE
Licha ya faida ya nyumbani, Tanzania inamenyana na Burkina Faso, timu yenye historia ndefu katika michuano ya CHAN na inayosifika kwa nidhamu na uchezaji wa mbinu. Huu unatafsiriwa kuwa mtihani muhimu kwa timu hiyo inayoongozwa na kocha wa Taifa Stars.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako