Kikosi cha Taifa Stars Leo Vs Niger 09/09/2025, Taifa Stars vs Niger Mechi ya Kufuzu Kombe la Dunia 2026: Taifa Stars inarejea nyumbani kuwakaribisha Niger katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026.
Baada ya sare ya ugenini, timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, inaendelea na kampeni yake ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026. Stars itashuka tena dimbani Jumanne hii kwenye Uwanja wa Amaan Complex mjini Zanzibar, ambapo itamenyana na Niger.
Mchezo huo muhimu umepangwa kufanyika saa 10:00 Jioni na unatarajiwa kuvuta hisia za mashabiki wengi wa soka nchini, hasa ikizingatiwa ushiriki wao katika hatua ya kwanza ya mchujo wa michuano hiyo mikubwa ya kimataifa.
Taifa Stars imesalia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya kucheza Kombe la Dunia 2026, na matokeo ya mechi hii yanaweza kuwa na athari kubwa kwenye msimamo wa makundi. Sare ya ugenini imewatia moyo wachezaji na makocha, lakini ushindi wa nyumbani utakuwa hatua muhimu kuelekea ndoto yao ya kucheza fainali za kimataifa.

Niger inasifika kwa ukakamavu na nidhamu ya ufundi, hivyo Taifa Stars itahitaji kucheza kwa umakini na kutumia vyema faida yao ya nyumbani. Miongoni mwa mambo yanayotarajiwa kuiinua Stars ni faida ya nyumbani, pamoja na hamasa ya mashabiki wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
Kikosi cha Taifa Stars Leo Vs Niger 09/09/2025
Kikosi kinachoaza leo
- Suleiman
- Kapombe
- Msindo
- Job
- Bacca
- NOVATUS
- Feis toto
- Mzize
- Seleman
- Msuva
- Samatta
SOMA PIA:
Weka maoni yako