KIKOSI Cha Yanga SC Leo vs Dodoma Jiji 22/06/2025 | Mechi Muhimu ya Hatima ya Ubingwa NBC Premier League.
Young Africans Sport Club (Yanga SC) inatarajiwa kushuka dimbani leo Jumapili Juni 22, 2025, Saa 10:00 Jioni kumenyana na Dodoma Jiji FC kwenye Uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara (NBC Premier League).
Yanga SC inayoongoza kwa sasa kwenye msimamo, inaelekea kwenye mechi hii ikiwa na lengo kuu moja: kusaka pointi tatu muhimu ili kujiweka katika nafasi nzuri na kutetea ubingwa wao wa ligi msimu huu. Ushindi wa leo utaipa Yanga SC nafasi nzuri zaidi ya kutawazwa bingwa, kutokana na matokeo ya wapinzani wao wakuu.
Dodoma Jiji FC iliyopo nafasi ya 9 kwenye msimamo, haiko kwenye hatari ya kushuka daraja bali inahitaji matokeo mazuri ili kuweza kupanda kutoka mkiani. Kwa hivyo, licha ya kutokuwa na shinikizo la hatima msimu huu, wataingia uwanjani wakiwa wamedhamiria kumaliza msimu kwa heshima.
KIKOSI Cha Yanga SC Leo vs Dodoma Jiji 22/06/2025
Kikosi cha Yanga kinachoaza leo dhidi ya Dodoma Jiji kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC, ikiwa ni mchezo wa kutamatisha pazia la Ligi Kuu Tanzania kwa msimu wa 2024/25:-
- MSHERY
- JOB
- BACCA
- BOKA
- KIBWANA
- MAXI
- ABUYA
- SUREBOY
- PACOME
- CHAMA
- MZIZE

CHECK ALSO:
Weka maoni yako