Kombe Jipya la Ligi ya Mabingwa Afrika CAF 2024/25

Kombe Jipya la Ligi ya Mabingwa Afrika CAF 2024/25: CAF itazindua kombe jipya la Ligi ya Mabingwa 2024/25 kwa ushirikiano na TotalEnergies.

SHIRIKISHO la Soka barani Afrika (CAF), kwa ushirikiano na TotalEnergies, limetangaza kuwa litazindua rasmi kombe jipya la TotalEnergies CAF Champions League kabla ya fainali ya msimu wa 2024/25.

Tukio la uzinduzi limepangwa Alhamisi, Mei 22, 2025, kuanzia saa 12:00 jioni. Saa za Afrika Mashariki (10:00 GMT), katika ofisi za TotalEnergies mjini Johannesburg, Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya CAF, kombe hilo jipya ni kipande cha kipekee cha fedha ambacho kinaashiria hadhi ya juu ya michuano hiyo na kitashirikiwa na klabu bingwa barani Afrika kuanzia msimu huu.

Kombe Jipya la Ligi ya Mabingwa Afrika CAF 2024/25

Kombe Jipya la Ligi ya Mabingwa Afrika CAF 2024/25
Kombe Jipya la Ligi ya Mabingwa Afrika CAF 2024/25

Tazama uzinduzi huo moja kwa moja

Shabiki yeyote anayetaka kutazama uzinduzi huo anaweza kuufuatilia moja kwa moja kupitia CAF TV, huku tukio hilo pia likirushwa na kituo cha televisheni cha Azamsport2 HD kinachorusha matangazo ya michezo mbalimbali barani Afrika.

CHECK ALSO: