Kombe la Muungano 2025 Kuchezwa Pemba, ZFF Yahamishia Mechi Uwanja wa Gombani: Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) limetangaza rasmi kuhamisha michuano ya Kombe la Muungano 2025 kutoka Uwanja Mpya wa Uwanja wa Amaan hadi Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba. Uamuzi huu umetokana na ushauri wa kitaalamu kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Kombe la Muungano 2025 Kuchezwa Pemba, ZFF Yahamishia Mechi Uwanja wa Gombani
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ZFF, CAF ilitoa maelekezo mahususi kwa njia ya barua pepe kuhusiana na hali ya Uwanja Mpya wa Uwanja wa Amaan Complex unaoendelea kujengwa na umeingia kwenye mfumo wa matumizi ya kiufundi chini ya uangalizi maalum. Hali ya uwanja bado haijakamilika, na muda zaidi unahitajika ili kuuimarisha kabla ya kuandaa mechi kadhaa mfululizo.
Kutokana na hali hiyo, CAF imependekeza michuano ya mwaka huu isichezwe uwanjani ili kulinda ubora wake na kuhakikisha usalama wa wachezaji. ZFF imetekeleza agizo hilo kwa kuhamishia rasmi mashindano hayo kwenye Uwanja wa Gombani, hatua inayoipa Pemba fursa ya kuandaa mashindano makubwa ya soka kitaifa.

Uamuzi huu unawapa fursa mashabiki wa soka wa Pemba kushuhudia michuano mingine mikubwa, na inatarajiwa kuongeza hamasa ya kimichezo na maendeleo ya miundombinu ya michezo katika eneo hilo.
ZFF imejipanga kuendelea kushirikiana kwa karibu na CAF na wadau wengine wa soka ili kuhakikisha michuano hiyo inafanyika kwa mafanikio na kufikia viwango vya kimataifa.
Kombe la Muungano ni moja ya mashindano ya kihistoria na yenye mvuto katika kalenda ya michezo ya Zanzibar, na uamuzi huu unalenga kudumisha ubora na uendelevu wake kwa kuzingatia viwango vya kitaaluma.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako