Kuelekea Mchezo wa Simba vs Stellenbosch, Kocha Fadlu Davids Asisitiza Umakini | Kocha wa Simba SC aonya dhidi ya ulevi kabla ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika 2024/25.
Kocha wa Simba SC, Fadlu Davids amesisitiza kuwa timu yake haitakiwi kulewa sifa au kushangilia mapema baada ya kufuzu kwa nusu fainali ya CAFCC. Badala yake, alisema waelekeze nguvu na mawazo yao yote katika mechi ya kesho dhidi ya Stellenbosch FC ya Afrika Kusini.
Kuelekea Mchezo wa Simba vs Stellenbosch, Kocha Fadlu Davids Asisitiza Umakini
“Tulisimamisha sherehe haraka” – Fadlu Davids
Akizungumza kabla ya mechi ya nusu fainali ya kwanza, itakayochezwa Jumamosi, Aprili 20, 2025, saa 10:00 jioni, kocha Fadlu alisema:
“Tulipofuzu kuingia nusu fainali, tulisitisha sherehe haraka. Kazi bado ni kubwa na tunapaswa kuikamilisha. Hatuwazii ubingwa kwa sasa; hilo ni jambo la mashabiki wetu. Sisi tunafikiria mpambano ujao.”
Maneno haya yanadhihirisha mtazamo wa kitaalamu na umakini ambao Simba SC wamejipanga nao kuelekea hatua muhimu ya mashindano haya ya CAF.

Ratiba ya Mchezo: Simba SC vs Stellenbosch FC
- Tarehe: Aprili 20, 2025
- Saa: 10:00 jioni (East Africa Time)
- Mahali: Taifa Stadium, Dar es Salaam
- Matangazo Mubashara: AzamSports1HD
CHECK ALSO:
Weka maoni yako