Liverpool Watwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England 2024/2025 | Liverpool FC imeweka historia kwa kushinda taji la Ligi Kuu ya Uingereza msimu wa 2024/2025 baada ya ushindi mnono wa mabao 5-1 dhidi ya Tottenham Hotspur kwenye Uwanja wao wa nyumbani, Anfield.
Kwa ushindi huu, Liverpool imefikisha pointi 82, idadi ambayo hakuna timu nyingine inaweza kufikia, licha ya mechi nne zilizosalia kumalizika kwa msimu. Hili ni taji la 20 la Premier League kwa Liverpool katika historia na linaimarisha hadhi yake kama moja ya vilabu vilivyo na mafanikio zaidi England.
Liverpool Watwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England 2024/2025
Ushindi huu haukutawaza tu mabingwa wa Liverpool, lakini pia ulionyesha kiwango cha juu cha uchezaji wao msimu huu chini ya uongozi dhabiti wa meneja wao.

FT: Liverpool 5-1 Tottenham Hotspur
⚽ 16’ Diaz
⚽ 24’ Mac Allister
⚽ 34’ Gakpo
⚽ 63’ Salah
⚽ 69’ Udogie
⚽ 12’ Solanke
Ubingwa wa Liverpool wa Ligi Kuu ya 2024/2025 ni dhihirisho la juhudi, umoja na ubora wa timu hiyo katika Ligi Kuu ya Uingereza. Mashabiki wa Majogoo wa Anfield wana kila sababu ya kujivunia msimu huu wenye mafanikio makubwa.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako