Lusajo Mwaikenda Aipeleka Azam Nusu Fainali ya Muungano Cup 2025: Katika mchezo mkali wa robo fainali ya Kombe la Muungano 2025, Azam FC ilifanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya KMKM ya Zanzibar.
Lusajo Mwaikenda Aipeleka Azam Nusu Fainali ya Muungano Cup 2025
Shujaa wa Azam FC katika mchezo huo alikuwa Lusajo Mwaikenda, aliyefunga bao pekee kwa kichwa baada ya kuunganisha kwa ustadi mpira wa kona wa Abdul Sopu. Bao hilo muhimu lilitosha kuipeleka Azam FC moja kwa moja kwenye nusu fainali ya michuano hiyo ya kihistoria.
Matokeo ya Mchezo:
KMKM 0 – 1 Azam FC
⚽ Mfungaji: Lusajo Mwaikenda – kwa kichwa, akimalizia kona ya Abdul Sopu

Kwa ushindi huo muhimu, Azam FC imedhihirisha kuwa iko tayari kuwania ubingwa wa Kombe la Muungano 2025. Ushirikiano mkubwa kati ya Sopu na Mwaikenda umetajwa kuwa moja ya chachu ya mafanikio ya klabu hiyo katika hatua za mwisho za mashindano hayo.
Azam FC sasa itacheza nusu fainali dhidi ya JKU iliyoitoa Singida Black Stars katika michuano hiyo iliyofanyika tarehe 28 kwenye Uwanja wa Gomba saa 1:15 usiku.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako