Mabadiliko ya Mitaala Kidato cha Sita ACSEE 2025

Mabadiliko ya Mitaala Kidato cha Sita ACSEE 2025: Masomo ya Lazima, Tahasusi na Utahini. Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) latangaza mfumo mpya wa mitihani ya darasa la sita (ACSEE)

Kwa kuzingatia Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014, Toleo la 2023, na mitaala iliyoboreshwa, Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza mabadiliko mapya ya taratibu za masomo na mitihani kwa wanafunzi wa darasa la sita (ACSEE).

Mabadiliko ya Mitaala Kidato cha Sita ACSEE 2025

Mabadiliko ya Mitaala Kidato cha Sita ACSEE 2025
Mabadiliko ya Mitaala Kidato cha Sita ACSEE 2025

Muundo Mpya wa Masomo kwa Kidato cha Sita:

✔ Mwanafunzi atatakiwa kusoma na kufanya mtihani wa masomo kati ya matano (05) hadi saba (07).
✔ Kati ya hayo:

  • Masomo ya lazima ni mawili (02)

  • Masomo ya tahasusi ni matatu (03)

  • Somo moja (01) la chaguo

  • Na somo la Basic Applied Mathematics (BAM) kwa tahasusi zinazohitaji somo hilo.

Masomo ya lazima ni pamoja na:

  • Historia ya Tanzania na Maadili

  • Academic Communication

Mfumo wa Mtihani ACSEE:
Mtahiniwa atafanya mitihani kwa mfumo ufuatao:

ACSEE (5-7) = Lazima (02) + Tahasusi (03) + Chaguzi (01)

Kwa hiyo, mwanafunzi atakuwa na machaguo matatu (03) ya muundo wa masomo kama ifuatavyo:

  • (2 + 3 + 0)

  • (2 + 3 + 1)

  • (2 + 3 + 1 + BAM)

✔ Ukokotoaji wa madaraja ya mwisho utazingatia masomo ya Tahasusi pekee.

CHECK ALSO: