Mahitaji ya JKT 2025 Vitu Muhimu vya Kwenda Navyo Kwa Waliochaguliwa JKT: Vifaa Muhimu kwa Vijana Watakaojiunga na JKT: Mwongozo Rasmi wa Kuripoti Makambini.
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limewaagiza vijana waliochaguliwa kujiunga na mafunzo yake kuhakikisha wanaripoti katika kambi hizo wakiwa na vifaa maalum vilivyoainishwa rasmi. Hii ni sehemu ya maandalizi muhimu ya kuanza kwa mafunzo ya kijeshi na uzalendo yanayotolewa na TDF.
Mahitaji ya JKT 2025 Vitu Muhimu vya Kwenda Navyo Kwa Waliochaguliwa JKT
Orodha ya vifaa vile ni kama ifuatavyo.

Bukta ya rangi ya βDark Blueβ β Inatakiwa iwe na mpira kiunoni (lastic), mfuko mmoja wa nyuma, na urefu unaofika magotini. Haipaswi kuwa na zipu.
T-shirt ya rangi ya kijani β Hii ni sehemu ya mavazi ya kawaida ya mafunzo.
Raba za michezo β Zenye rangi ya kijani au blue (bluu), zinazofaa kwa shughuli za mazoezi.
Shuka mbili za kulalia β Zenye rangi ya blue bahari, kwa matumizi ya kulala kambini.
Soksi ndefu β Za rangi nyeusi, zinazofaa kwa matumizi ya kila siku katika mazingira ya kijeshi.
Nguo za kuzuia baridi β Hii ni kwa wale waliopangiwa makambi yaliyopo katika mikoa yenye hali ya hewa ya baridi.
Track suit β Ya rangi ya kijani au blue, kwa ajili ya mazoezi ya kila siku.
Nyaraka muhimu za udahili β Ikiwemo vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya kuhitimu Elimu ya Sekondari (kidato cha nne) pamoja na vyeti vingine vinavyohitajika kwa kujiunga na elimu ya juu.
Nauli ya kwenda na kurudi β Kila kijana anapaswa kuwa na fedha ya nauli kwa ajili ya kwenda kuripoti makambini na kurejea nyumbani baada ya mafunzo.
Vijana wanakumbushwa kufuata maagizo haya kwa uangalifu ili kuepuka usumbufu au kuchelewa wanapofika kambini. Kukosa kufuata mahitaji haya kunaweza kusababisha kutokubalika au kucheleweshwa kwa kuanza rasmi kwa mafunzo/Mahitaji ya JKT 2025 Vitu Muhimu vya Kwenda Navyo Kwa Waliochaguliwa JKT.
ANGALIA HAPA MAJINA
CHECK ALSO:
Weka maoni yako