Majibu Rasmi Kuhusu Madai ya Timu Kugomea Ligi Kuu Tanzania Bara | Imeripotiwa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuwa baadhi ya klabu zinazoshiriki Ligi Kuu ya NBC zimeiandikia barua Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) kueleza kutoridhishwa kwao na maamuzi na uendeshaji wa ligi hiyo. Pia imedaiwa kuwa baadhi ya timu zinapanga kuketi mechi mbili za mwisho.
Majibu Rasmi Kuhusu Madai ya Timu Kugomea Ligi Kuu Tanzania Bara
Hata hivyo, taarifa rasmi kutoka kwa mamlaka husika zinaonyesha kuwa hakuna barua iliyopokelewa kuthibitisha madai hayo/Majibu Rasmi Kuhusu Madai ya Timu Kugomea Ligi Kuu Tanzania Bara.
Taarifa ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB)
Afisa Habari wa TPLB, Bw. Karim Boimanda, amesema kwa uwazi kuwa:
“Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) haijapokea barua yoyote kutoka kwa timu yoyote ile ya Ligi Kuu ya NBC wala NBC Championship. Hata hao Singida Black Stars, licha ya msemaji wao kuzungumza na vyombo vya habari, bado hatujapokea barua rasmi ya malalamiko kutoka kwao.”
Kauli hii inaweka bayana kuwa hadi sasa, hakuna msingi wa kisheria au kiutendaji unaoweza kuthibitisha kuwepo kwa mgogoro rasmi kati ya klabu hizo na TPLB.

Taarifa ya Baraza la Michezo Tanzania (BMT)
Kwa upande wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Katibu Mkuu Bi. Neema Msitha ameeleza wakati wa mahojiano na kipindi cha Crown Sports kupitia 92.1 Crown FM kuwa:
“Hatujapokea barua wala nakala yoyote ya timu ya Ligi Kuu ya NBC kugomea michezo miwili ya mwisho ya ligi hiyo.”
Utafiti wa Waandishi wa Habari
Mwandishi wa habari maarufu nchini na mchambuzi wa masuala ya michezo Nassibu Mkomwa, naye amefanya ufuatiliaji kwa kina kwa kuzungumza na Watendaji Wakuu (CEOs) wa timu 13 kati ya 16 zinazoshiriki Ligi Kuu ya NBC. Kwa mujibu wa taarifa yake:
“Hakuna kiongozi hata mmoja aliyekiri kuwa ameandika barua ya kugomea michezo miwili iliyobaki. Kwa kweli, wengi wao wamesema timu zao zipo kambini na zinaendelea na maandalizi ya michezo hiyo.”
Kwa kuzingatia taarifa hizi zote kutoka kwa mamlaka rasmi na waandishi wa habari wanaoaminika, inaonekana kwamba madai ya klabu hiyo kususia ligi au kuwasilisha barua ya malalamiko bado hayajathibitishwa rasmi.
Wadau wa soka, mashabiki, na vyombo vya habari wanashauriwa kuwa waangalifu kuhusu habari zinazosambazwa bila uthibitisho rasmi. Ni muhimu kuepuka kueneza au kuamini taarifa ambazo hazijathibitishwa na mamlaka husika ili kulinda heshima na utulivu wa ligi.
TPLB na BMT zinaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa ligi na kuhakikisha kuwa michuano hiyo inamalizika kwa amani, haki na usawa kwa timu zote shiriki/Majibu Rasmi Kuhusu Madai ya Timu Kugomea Ligi Kuu Tanzania Bara.
ANGALIA PIA:
Weka maoni yako