Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Utumishi wa Umma Aprili 2025, TANGAZO LA USAILI: Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Utumishi wa Umma Aprili 2025
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, pamoja na Taasisi na Mamlaka nyingine za Serikali (MDAs & LGAs), ametangaza orodha ya waombaji kazi walioteuliwa kuhudhuria usaili utakaoanza tarehe 14 Aprili 2025 hadi 18 Aprili 2025.
Usaili huu utafanyika katika vituo mbalimbali vilivyopangwa kulingana na kada za kazi walizoomba. Waombaji wote wanaoitwa kwenye usaili huo wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:
Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Utumishi wa Umma Aprili 2025

Maelekezo Muhimu kwa Waombaji:
Usaili utafanyika kwa tarehe na muda uliowekwa kwenye tangazo rasmi kwa kila kada.
Kila mshiriki anatakiwa kuvaa barakoa (mask) anapofika eneo la usaili.
Kila mshiriki ni lazima awe na kitambulisho kwa ajili ya utambulisho.
Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:
Kitambulisho cha Mkaazi
Kitambulisho cha Mpiga kura
Kitambulisho cha Kazi
Kitambulisho cha Uraia
Hati ya kusafiria
Leseni ya Udereva
Barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa au kijiji.
Waombaji wanapaswa kuja na vyeti vyao halisi, ikiwa ni pamoja na:
Cheti cha kuzaliwa
Vyeti vya kidato cha IV, VI
Astashahada
Stashahada
Shahada ya juu kulingana na sifa za nafasi ya kazi.
Vyeti feki au vya muda kama Testimonial, Provisional Results, au matokeo ya Form IV na VI (statement of results) havitaruhusiwa.
Kila mshiriki atajigharamia chakula, usafiri, na malazi.
Mshiriki asipofika siku ya usaili kama ilivyoainishwa, atakuwa amepoteza nafasi.
Waombaji waliomaliza nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na TCU, NACTE au NECTA.
Waombaji ambao majina yao hayajaonekana kwenye tangazo hili wanatakiwa kuelewa kuwa hawakukidhi vigezo. Hawatopangiwa tena nafasi hadi nafasi mpya zitakapotangazwa.
MAJINA HAYA HAPA
Waombaji wanakumbushwa kuzingatia maelekezo yote yaliyotolewa. Kukosa cheti halisi, kutokuvaa barakoa au kutofika siku ya usaili kunaweza kusababisha kufutiwa kwa nafasi hiyo ya kazi.
Kwa majina ya walioitwa na ratiba kamili ya usaili, tafadhali tembelea tovuti rasmi ya Sekretarieti ya Ajira: www.ajira.go.tz
Weka maoni yako