Makundi ya Mapinduzi Cup 2025/2026 | MAPINDUZI CUP 2026: Makundi na Viwanja Rasmi vya Mashindano.
Makundi ya Mapinduzi Cup 2025/2026
Mashindano ya Mapinduzi Cup 2026 yamepangwa rasmi kuanza tarehe 28 Desemba 2025 na yanatarajiwa kumalizika tarehe 13 Januari 2026. Michuano hii ni sehemu muhimu ya kalenda ya soka Tanzania, ikiwaleta pamoja vilabu vikubwa vya Tanzania Bara na Zanzibar, pamoja na taasisi za kijeshi.
Makundi
Mapinduzi Cup 2026 imeundwa kwa makundi matatu, kila kundi likiwa na timu tatu hadi nne kama ifuatavyo:
Kundi A
- Mlandege FC
- Azam FC
- Singida Black Stars
- Ura FC
Kundi B
- Simba SC
- Muembe Makumbi City
- Fufuni SC
Kundi C
- Yanga SC
- KVZ
- TRA
Timu zitacheza hatua ya makundi kabla ya kuingia hatua ya nusu fainali na fainali.

Viwanja Vitakavyotumika
Mashindano yote yatafanyika Zanzibar katika viwanja viwili rasmi:
-
Uwanja wa Amaan, Unguja
-
Uwanja wa Gombani, Pemba
Hatua kubwa ya makundi na nusu fainali zitachezwa Amaan Stadium, huku fainali ikipangwa kuchezwa Gombani Stadium.
CHECK ALSO:








Weka maoni yako