Mambo 6 Waislamu Wanapaswa Kufanya Kabla na Baada ya Sala ya Eid ul-Fitr 2025

Mambo 6 Waislamu Wanapaswa Kufanya Kabla na Baada ya Sala ya Eid ul-Fitr 2025: Saudi Arabia imetangaza rasmi kuwa Eid Al-Fitr 2025 itaadhimishwa Jumapili, Machi 30, 2025, kufuatia kuthibitishwa kuonekana kwa mwezi. Huu ni mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na mwanzo wa sherehe za Eid.

Waislamu kote ulimwenguni husherehekea Eid kwa ibada na furaha. Swala ya Eid ni mojawapo ya ibada muhimu sana katika siku hii, na kuna mambo kadhaa Waislamu wanatakiwa kufanya kabla na baada ya sala.

Mambo 6 Waislamu Wanapaswa Kufanya Kabla na Baada ya Sala ya Eid ul-Fitr 2025

1. Kutoa Zakat al-Fitr

  • Zakat al-Fitr ni sadaka ya chakula inayotolewa mwishoni mwa Ramadhani kwa ajili ya kusaidia masikini.

  • Inapaswa kutolewa kabla ya Sala ya Eid, kwa mujibu wa mafundisho ya Mtume Muhammad (S.A.W).

  • Lengo lake ni kuwatakasa Waislamu waliokuwa wakifunga na kuhakikisha kuwa masikini nao wanashiriki furaha ya Eid.

2. Kuoga Kabla ya Sala ya Eid

  • Ni Sunnah kuoga kabla ya kwenda kuswali, ili kuwa safi kwa ibada hii muhimu.

  • Inapendekezwa pia kwa wanaume kutumia manukato mazuri kabla ya kwenda msikitini.

3. Kula Kabla ya Kuswali Sala ya Eid

  • Mtume Muhammad (S.A.W) alihimiza kula tende au chakula kingine cha halali kabla ya kwenda kuswali Eid al-Fitr.

  • Hii ni alama ya kuashiria kuwa mfungo wa Ramadhani umemalizika.

4. Kusema Takbir Wakati wa Kwenda Kusali

  • Ni Sunnah kusema Takbir wakati wa kuelekea msikitini hadi sala ya Eid itakapoanza.

  • Takbir inasema:
    “Allahu Akbar, Allahu Akbar, Lailaha illahahu Wallahu Akbar, Allahu Akbar Walillahil Hamd.”

Mambo 6 Waislamu Wanapaswa Kufanya Kabla na Baada ya Sala ya Eid ul-Fitr 2025
Mambo 6 Waislamu Wanapaswa Kufanya Kabla na Baada ya Sala ya Eid ul-Fitr 2025

5. Kusikiliza Hutba Baada ya Sala ya Eid

  • Baada ya swala, hutuba hutolewa, na waumini wanashauriwa kusikiliza badala ya kuondoka mara moja.

  • Ingawa hutuba si wajibu, ni sehemu muhimu ya kupata mafundisho ya kidini.

6. Kubadilisha Njia Unaporudi Nyumbani

  • Mtume Muhammad (S.A.W) alihimiza kubadilisha njia unaporejea kutoka Sala ya Eid.

  • Hii ni njia ya kusalimiana na watu wengi zaidi na kueneza furaha ya Eid.

Eid ni siku ya shukrani, furaha, na mshikamano wa kijamii. Waislamu wanahimizwa kusherehekea kwa kuheshimu maadili ya kidini, kusaidiana na kuepuka vitendo vinavyokiuka mafundisho ya Kiislamu/Mambo 6 Waislamu Wanapaswa Kufanya Kabla na Baada ya Sala ya Eid ul-Fitr 2025.

CHECK ALSO: