Mamelodi Sundowns vs Pyramids Jumamosi Hii, Fainali ya CAF Champions League 2025: Jumamosi hii, Mei 24, 2025, mashabiki wa soka barani Afrika watashuhudia mpambano wa kusisimua kati ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na Pyramids FC ya Misri katika mkondo wa kwanza wa fainali ya Ligi ya Mabingwa ya CAF ya 2024/2025.
Mamelodi Sundowns vs Pyramids Jumamosi Hii, Fainali ya CAF Champions League 2025
Mechi hii itachezwa kwenye Uwanja wa Loftus Versfeld mjini Pretoria, kuanzia saa 10:00 jioni. Saa za Afrika Mashariki (EAT). Mashabiki wanaweza kuitazama moja kwa moja kupitia Azam Sports 1 HD, ambayo itarusha mechi hiyo kwa ubora wa hali ya juu.
Hii ni mara ya kwanza kwa Pyramids FC kufika fainali ya michuano hii, jambo linaloonyesha ukuaji mkubwa wa soka nchini Misri na uwekezaji mkubwa katika timu hiyo. Kwa Mamelodi Sundowns, hii ni fursa nyingine ya kihistoria ya kuongeza taji lingine kwa mafanikio yao ya 2016.
Fainali hii ya kwanza inatarajiwa kuwa na upinzani mkali, kwa kuzingatia ubora wa timu zote mbili. Wadau wa soka, wachambuzi, na mashabiki wana matarajio makubwa ya uchezaji na nidhamu ya hali ya juu uwanjani.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako