Manchester United vs Tottenham Fainali ya Europa League 2025: Manchester United na Tottenham Zatinga Fainali ya Europa League 2025.
Manchester United na Tottenham Hotspur zimefuzu rasmi kwa fainali ya UEFA Europa League 2024/2025 baada ya ushindi wa kuvutia wa nusu fainali dhidi ya Athletic Bilbao na Bodo/Glimt mtawalia.
Manchester United vs Tottenham Fainali ya Europa League 2025
Katika mechi ya mkondo wa pili, Mei 8, 2025, Manchester United ilishinda 4-1 dhidi ya Athletic Bilbao, na kuacha matokeo ya jumla kuwa 7-1 baada ya mikwaju miwili ya penalti katika nusu fainali. Mabao ya United yalifungwa na Mason Mount (72′ na 90+1′), Casemiro (80′), na Rasmus Hojlund (85′), huku Athletic wakifunga bao la kufutia machozi kupitia kwa Jauregizar dakika ya 31.
FT: Man United 🏴 4-1 🇪🇸 Athletic Bilbao (Agg. 7-1)
⚽ 72’ Mount
⚽ 80’ Casemiro
⚽ 85’ Hojlund
⚽ 90+1’ Mount
31’ Jauregizar ⚽
Kwa upande mwingine, Tottenham walionyesha ubora wao kwa kuwalaza Bodo/Glimt 2-0 ugenini, na kusonga mbele kwa jumla ya 5-1. Dominic Solanke alitangulia kufunga dakika ya 63, na Pedro Porro akakamilisha kazi dakika ya 69/Manchester United vs Tottenham Fainali ya Europa League 2025.
FT: Bodo/Glimt 🇳🇴 0-2 🏴 Tottenham (Agg. 1-5)
⚽ 63’ Solanke
⚽ 69’ Porro
Fainali inayosubiriwa kwa hamu itachezwa Mei 21, 2025, kwenye Uwanja wa San Mamés mjini Bilbao, Uhispania, ambapo timu zote za Uingereza zitamenyana kuwania kombe la pili kwa ukubwa barani Ulaya.

Fainali hii kati ya Manchester United na Tottenham inatarajiwa kuwa ya kihistoria, huku kila timu ikitafuta ushindi wa heshima na nafasi ya kushiriki michuano ya UEFA Super Cup. Mashabiki wa soka duniani kote wana matarajio makubwa kwa mechi yenye ushindani mkali na burudani ya hali ya juu.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako