Matokeo Simba vs Nsingizini Leo 26/10/2025, Mnyama Kuwakaribisha Wageni wa Eswatini Benjamin Mkapa Saa 10:00 Jioni.
Jumapili hii hisia za mashabiki wa soka wa Tanzania zitaelekezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, ambapo wenyeji Simba SC watamenyana na Nsingizini Hotspurs ya Eswatini katika mchezo wa mkondo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika 2025/26.
Simba SC inasonga mbele kwa mabao matatu kwa moja (3-0) baada ya kufunga katika mchezo wa mkondo wa kwanza huko Eswatini. Matokeo haya yanawaweka katika nafasi nzuri ya kufuzu kwa hatua ya makundi ya kinyang’anyiro cha kwanza cha vilabu barani Afrika.
Wachezaji wa Simba SC wanatarajiwa kushuka uwanjani wakiwa na ari kubwa baada ya kupata ushindi mnono katika mchezo wa kwanza. Kocha wa timu hiyo amesisitiza umuhimu wa kuendelea kudhibiti mechi ili kuhakikisha timu inapata matokeo chanya na kufuzu rasmi hatua ya makundi.

Kwa upande mwingine, Nsingizini anatarajiwa kupambana kwa nguvu zake zote kurekebisha makosa yaliyofanyika nyumbani. Hata hivyo, changamoto yake kubwa itakuwa ni kuhimili presha ya mashabiki wa Simba ambao huwa wanajazana kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Matokeo Simba vs Nsingizini Leo 26/10/2025
LIVE | SIMBA SC -:- NSINGIZINI HOTSPURS
Ushindi wowote au sare yoyote katika mechi hii itaiwezesha Simba SC kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua muhimu kwa klabu hiyo inayopania kufanya vyema kimataifa msimu huu.
Timu hiyo imeonyesha ubora wa hali ya juu katika mechi zilizopita, na mashabiki wake wanatarajia kuona muendelezo wa matokeo hayo mazuri hasa kwenye uwanja wao wa nyumbani/Matokeo Simba vs Nsingizini Leo 26/10/2025.
Mashabiki wa Simba wameshauriwa kufika uwanjani mapema ili kuepuka mikusanyiko ya watu na kuheshimu kanuni za usalama. Sambamba na hayo, wanakumbushwa kuendelea kuisapoti timu yao kwa nidhamu na utulivu, ili siku hii iwe ya kihistoria kwa Wanyama.
CHECK ALSO:







Weka maoni yako