Matokeo ya Azam FC vs Mbeya City Leo 24/09/2025 Saa 3 Usiku | Mchezo wa Kwanza Ligi Kuu NBC 2025/26. Azam FC Yaanza Msimu Mpya wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mbeya City
Msimu mpya wa 2025/26 wa ligi kuu ya NBC Tanzania bara unaendelea. Leo Jumatano Septemba 24, 2025 Azam FC wataanza rasmi kampeni zao dhidi ya Mbeya City.
Mchezo huo utapigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, kuanzia saa 3:00 Usiku.
Azam FC: Timu hiyo inatarajiwa kutumia mechi hii kuonyesha ubora wao na kuanza msimu mpya kwa ushindi, ikizingatiwa kuwa wameimarisha msimu wao kwa usajili na maandalizi ya msimu mpya.
Mbeya City: Ikiwa na historia ya kuwa mwiba kwa timu kubwa, klabu hii inatarajiwa kushuka dimbani ikiwa na ari kubwa ya kupata matokeo chanya dhidi ya Azam.
Matokeo ya Azam FC vs Mbeya City Leo 24/09/2025
LIVE | AZAM -:- MBEYA CITY

Mashabiki wa soka wanatarajia mechi yenye ushindani mkubwa kutokana na matokeo ya timu zote mbili kwenye ligi. Azam ikicheza nyumbani itashuka uwanjani ikiwa na hamu ya kuanza msimu ikiwa na pointi tatu, huku Mbeya City ikisaka ushindi wa kwanza ili kuongeza morali mwanzoni mwa msimu.
Mchezo wa leo usiku wa Azam FC dhidi ya Mbeya City unatarajiwa kuteka hisia za mashabiki wa soka nchini. Timu zote mbili zinakutana kwa malengo tofauti, lakini ushindi ni kipimo cha kwanza cha mafanikio yao katika msimu wa 2025/26 wa Ligi Kuu ya NBC.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako