Matokeo ya Darasa la Saba na Shule Walizopangiwa 2025/2026, Matokeo Darasa La Saba 2025/2026.
Matokeo ya Darasa la Saba na Shule Walizopangiwa 2025/2026
Serikali imethibitisha kuwa jumla ya wanafunzi 937,581, sawa na asilimia 100 ya waliohitimu darasa la saba mwaka 2025 na kupata alama kati ya 121 hadi 300, wamechaguliwa kuanza masomo ya kidato cha kwanza mwaka 2026. Taarifa hii imetolewa Desemba 4, 2025 na Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Profesa Riziki Shemdoe, katika mkutano na waandishi wa habari.
Uchaguzi huu umefanyika kwa kuzingatia miongozo ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, ikihakikisha kila mwanafunzi mwenye sifa anapata nafasi katika shule za Serikali.
Mgawanyo wa Wanafunzi Waliochaguliwa
Takwimu rasmi zinaonyesha mgawanyo ufuatao:
-
Wasichana: 508,477
-
Wavulana: 429,104
-
Wenye Mahitaji Maalum: 3,228 (Wasichana 1,544; Wavulana 1,684)
-
Jumla ya Shule Walizopangiwa: Shule za Sekondari za Serikali 5,230
BOFYA HAPA KUONA ORODHA YA WANAFUNZI WALIOPANGWA KWENDA SHULE MOJA
ARUSHA |
DAR ES SALAAM |
DODOMA |
GEITA |
IRINGA |
KAGERA |
KATAVI |
KIGOMA |
KILIMANJARO |
LINDI |
MANYARA |
MARA |
MBEYA |
MOROGORO |
MTWARA |
MWANZA |
NJOMBE |
PWANI |
RUKWA |
RUVUMA |
SHINYANGA |
SIMIYU |
SINGIDA |
SONGWE |
TABORA |
TANGA |
Aidha, makundi maalum ya wanafunzi yamepangwa kama ifuatavyo:
1. Shule za Wenye Ufaulu wa Juu
Wanafunzi 815 (Wasichana 335; Wavulana 480) wamechaguliwa kujiunga na shule zenye historia ya kufanya vizuri kitaaluma kama: (Shule Walizopangiwa Form One 2026)
-
Ilboru
-
Msalato
-
Kibaha
-
Kilakala
-
Mzumbe
-
Tabora Boys
-
Tabora Girls
2. Shule za Amali za Bweni
Jumla ya 3,411 wamepangwa kwenye shule hizi, ikiwa ni:
-
Wasichana: 1,279
-
Wavulana: 2,162
3. Shule za Bweni za Kitaifa
Wanafunzi 7,360 wamepangwa katika shule hizi, wakiwemo:
-
Wasichana: 5,014
-
Wavulana: 2,346
4. Shule za Sekondari za Kutwa
Hiki ndicho kikundi kikubwa zaidi, chenye wanafunzi 925,065:
-
Wasichana: 501,849
-
Wavulana: 424,116
Hawa wote watasoma katika shule za kutwa zilizo karibu na maeneo yao ya makazi.

Uteuzi wa wanafunzi 937,581 kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2026 unaonyesha dhamira ya Serikali kusimamia upatikanaji wa elimu bila malipo kwa watoto wote wenye sifa. Ushirikiano wa wazazi, jamii na taasisi za elimu utahitajika ili kuhakikisha wanafunzi wanaanza masomo kwa wakati na kupata mazingira mazuri ya kujifunzia.
CHECK ALSO:






Saf kabisa hongera watoto wetu
Matokeo ya ngasaro primary school 2025
matokeo ya arusha primay school 2025