Matokeo ya Kidato cha Nne 2025/2026 CSEE NECTA | Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika kuanzia Novemba 11 hadi 29, 2024.
Matokeo hayo yametangazwa leo Ijumaa Januari 23, 2025 na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Said Mohammed.
Matokeo ya Kidato cha Nne 2025/2026 CSEE NECTA
Jumla ya watahiniwa 557,796 walisajiliwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne wakiwemo Wasichana 296,051 (53.08%) na Wavulana 261,745 (46.92%). Kati ya watahiniwa 557,796 waliosajiliwa, watahiniwa wa Shule walikuwa 529,329 na watahiniwa wa Kujitegemea walikuwa 28,467.

Kati ya watahiniwa 529,329 wa Shule waliosajiliwa, watahiniwa 517,460 sawa na asilimia 97.76 walifanya mtihani ambapo Wasichana walikuwa 271,918 sawa na asilimia 97.54 ya Wasichana wote huku Wavulana wakiwa 245,542 sawa na asilimia 98.00 ya Wavulana wote. Watahiniwa 11,869 sawa na asilimia 2.24 hawakufanya Mtihani.
Kati ya watahiniwa 28,467 wa Kujitegemea waliosajiliwa, watahiniwa 25,151 sawa na asilimia 88.35 walifanya Mtihani na watahiniwa 3,316 sawa na asilimia 11.65 hawakufanya Mtihani.
MATOKEO YALIYOPITA
2024
2023
2022
CHECK ALSO:







Weka maoni yako