MATOKEO ya Mtibwa Sugar vs Mbeya City Leo 15/05/2025: Mechi Maalum ya Kukabidhi Kombe la Ubingwa Championship 2024/2025.
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kuwa kutakuwa na mechi maalum ya kukabidhi kombe la Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (Ubingwa) msimu wa 2024/2025, ambapo Mtibwa Sugar itamenyana na Mbeya City FC katika mchezo wa kihistoria.
MATOKEO ya Mtibwa Sugar vs Mbeya City Leo 15/05/2025
Mtibwa Sugar iliyong’ara msimu huu kwenye michuano hiyo, imetangazwa rasmi kuwa mabingwa wa Ligi Daraja la Kwanza baada ya kuongoza msimamo wa ligi hiyo kwa kuwa na pointi nyingi zaidi. Mbeya City ambayo msimu huu nayo imetamba msimu huu itakuwa ni mpinzani anayestahili katika mechi hii maalum.

Mechi hii inalenga kumaliza msimu wa Ubingwa kwa heshima na hadhi inayostahili. Mtibwa Sugar itapokea kombe la ubingwa mbele ya mashabiki, wadau wa soka, na viongozi wa TFF. Tukio hili linadhihirisha dhamira ya TFF katika kutambua mafanikio ya timu zinazofanya vizuri katika ligi za maendeleo.
Mchezo kati ya Mtibwa Sugar na Mbeya City unatarajiwa kuwa ishara ya heshima na kilele cha mafanikio ya Mtibwa Sugar katika msimu wa Michuano wa 2024/2025. Tukio hili si la kukosa, kwani linatoa fursa ya kusherehekea maendeleo ya soka la ndani na kutambua juhudi za timu zinazojitolea.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako