Matokeo ya Usaili wa Ajira TRA 2025

Matokeo ya Usaili wa Ajira TRA 2025 | Ratiba ya Mahojiano ya Vitendo na Mahojiano Yametolewa

Dar es Salaam, Aprili 2, 2025 – Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetangaza matokeo ya usaili wa maandishi kwa waombaji kazi uliofanyika Machi 29 na 30, 2025, yatatolewa rasmi Aprili 25, 2025. Taarifa hii imetolewa leo na Mkurugenzi wa Usimamizi na Utawala wa Rasilimali Watu wa TRA, Moshi Kabengwe.

Kulingana na Kabengwe, matokeo yatatolewa baada ya kupokea matokeo kutoka kwa mshauri wa taaluma aliyesimamia zoezi la usaili, ambaye anatarajiwa kuwasilisha ripoti yake Aprili 23, 2025.

Matokeo ya Usaili wa Ajira TRA 2025

Ratiba ya Usaili wa Vitendo na Mahojiano

Baada ya kutangazwa kwa matokeo ya usaili wa maandishi, hatua zinazofuata ni usaili wa vitendo na mahojiano. Kabengwe ameeleza kuwa:

  • Usaili wa vitendo: Utafanyika kuanzia Mei 2 hadi 4, 2025 kwa kada za madereva na waandishi waendesha ofisi.

  • Usaili wa mahojiano: Utafanyika kuanzia Mei 7 hadi 9, 2025 kwa kada nyingine zote.

Mafunzo Rasmi ya Ajira na Mwelekeo

Watahiniwa watakaofaulu majaribio ya vitendo na usaili watapata taarifa rasmi ya ufaulu wao tarehe 18 Mei, 2025. Aidha, mafunzo elekezi kwa watumishi watarajiwa yataanza tarehe 22 Mei hadi Juni 2, 2025 na baada ya hapo watumishi wapya wataanza kazi rasmi ndani ya TRA.

Matokeo ya Usaili wa Ajira TRA 2025
Matokeo ya Usaili wa Ajira TRA 2025

Takwimu Muhimu Kuhusu Mchakato

  • Jumla ya maombi yaliyokidhi vigezo vilikuwa 112,952.
  • Maombi 71 ya nyongeza yalipokelewa kupitia rufaa, na kufikisha jumla ya 113,023 kutoka kwa waombaji 86,314.
  • Watahiniwa 78,544 walishiriki usaili wa maandishi, sawa na asilimia 91 ya waombaji wote.
  • Waombaji 7,770 (asilimia 9) hawakufika kwenye usaili kwa sababu mbalimbali.

Kabengwe alisisitiza kuwa mchakato wa ajira unafanyika kwa uwazi, usawa na kwa kuzingatia sifa za kitaaluma bila kujali hadhi ya mwombaji kijamii. Aliongeza kuwa vituo vya usaili vilisambazwa katika mikoa minane na Zanzibar ili kuruhusu waombaji kutoka maeneo mbalimbali kupata huduma kwa urahisi.

Waombaji wote wanashauriwa kufuata taarifa rasmi za TRA kupitia tovuti yake www.tra.go.tz au vyombo vya habari vilivyoidhinishwa, na kuepuka kutegemea taarifa ambazo hazijathibitishwa mtandaoni/Matokeo ya Usaili wa Ajira TRA 2025.

CHECK ALSO: