Mechi ya Simba vs RS Berkane Kupigwa Zanzibar Mei 25, 2025: Simba SC imethibitisha kuwa mechi dhidi ya RS Berkane itafanyika Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar Mei 25, 2025.
Uongozi wa Simba SC umetoa taarifa rasmi kwa umma ikionyesha kuwa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Simba SC na RS Berkane haitachezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kama ilivyopangwa awali. Pamoja na jitihada mbalimbali za Serikali, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), na klabu yenyewe, jitihada hizo hazikufanikiwa, na mechi hiyo haikuweza kuchezwa jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Simba SC, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limeamuru mchezo huo ufanyike kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar Mei 25, 2025. Uongozi wa klabu hiyo umewataka mashabiki kuwa watulivu wakati huu, huku wakiahidi kutoa taarifa rasmi kuhusiana na maandalizi ya mechi hiyo na mipango ya mashabiki kuelekea mechi hiyo muhimu.
Mechi ya Simba vs RS Berkane Kupigwa Zanzibar Mei 25, 2025
Taarifa hizo zitatangazwa katika mkutano maalum na waandishi wa habari utakaofanyika kesho Mei 20, 2025, saa 11:00 asubuhi katika ofisi za Klabu ya Simba zilizopo Oysterbay, Dar es Salaam.
Mashabiki wanashauriwa kufuata matangazo rasmi ya klabu kwa taarifa sahihi kuhusu usafiri, tikiti na mipango mingine. Epuka taarifa zisizo rasmi za mtandaoni ambazo zinaweza kupotosha au kusababisha mkanganyiko.
CHECK ALSO:
- Yanga Yatinga Fainali ya CRDB Cup Baada ya Ushidi Vs JKT Tanzania 2-0
- Azizi Ki Kucheza Mchezo Wake wa Mwisho Yanga SC Leo Dhidi ya JKT Tanzania
- Simba Yawasili Tanzania Kutokea Morocco, Maandalizi ya Mchezo wa Marudiano Yaaza
- Waamuzi Mechi ya Yanga Leo vs JKT Tanzania CRDB Federation Cup 2024/2025 Nusu FainaliÂ
Weka maoni yako