Mguto Asema Kesi ya Yanga 2021 Ilikuwa Kubwa Kuliko ya Simba

Mguto Asema Kesi ya Yanga 2021 Ilikuwa Kubwa Kuliko ya Simba, ilipaswa kushushwa daraja” Steven Mguto: Kesi ya Yanga mwaka 2021 kugomea kucheza mechi ilikuwa nzito kuliko ile ya Simba na ilipaswa kuadhibiwa vikali.

Mguto Asema Kesi ya Yanga 2021 Ilikuwa Kubwa Kuliko ya Simba

Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) Steven Mguto ameweka wazi kuwa sakata la kugomea Yanga SC mwaka 2021 lilikuwa kubwa kuliko la sasa linaloihusu Simba SC.

Kwa mujibu wa Mguto, iwapo kanuni na sheria za ligi zingefuatwa hadi kufikia hatua hiyo, Yanga SC ingepata adhabu kali ikiwamo kupoteza pointi tatu na hata kushuka daraja.

“Suala la Yanga mwaka 2021 lilikuwa kubwa kuliko la Simba, kwa kweli kwa mujibu wa sheria walipaswa kupoteza pointi na hata kushushwa daraja,” alisema Mguto na kuongeza kuwa uamuzi wa mwisho wa TPLB unatanguliza masilahi ya soka na mashabiki wake.

Kauli hii imezua mjadala kwa mashabiki wa soka nchini, huku wengi wakisubiri kwa hamu maamuzi ya mwisho kuhusiana na mgogoro wa Simba SC unaoendelea/Mguto Asema Kesi ya Yanga 2021 Ilikuwa Kubwa Kuliko ya Simba.

Mguto Asema Kesi ya Yanga 2021 Ilikuwa Kubwa Kuliko ya Simba
Mguto Asema Kesi ya Yanga 2021 Ilikuwa Kubwa Kuliko ya Simba

Tamko la Mwenyekiti kwenye taharuki hii

Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Steven Mnguto, amesema tayari wamejibu barua ya Yanga na hawana mamlaka ya kuwazuia kwenda CAS lakini kama wameenda CAS kwa kipindi hiki ambapo hawajasema kuwa suala hilo limeamriwa vipi itakuwa ni kitu cha kuchekesha.

Akisisitiza kuwa maamuzi ya mwisho ya bodi bado hayajatolewa, akiamini kuwa suluhu inaweza kupatikana kupitia vikao vya ndani. Mnguto ameeleza kuwa busara na hekima zinapaswa kutumika ili kila upande uridhike badala ya kupeleka suala hilo nje ya nchi.

”Hili jambo lazima hekima na busara itumike, Sheria, kanuni zipo kweli lakini lazima pia utumie hekima na busara, huyo asiyetaka kutumia hekima wala busara kusema kweli huyo hayupo upande wetu kutatua hilo tataizo. Nia yake ni kutengeneza tatizo jipya ambalo haitakuwa na maana yoyote, hata kuziombea timu moja kushushwa daraja unapata faida gani?” – Steven Mnguto

CHECK ALSO: