Misri Yatinga Nusu Fainali Baada, Ushindi wa 3-2 Vs Ivory Coast | Mabingwa watetezi wa Kombe la Mataifa Afrika (AFCON), Ivory Coast maarufu kama The Elephants, wameaga rasmi michuano ya AFCON 2025 baada ya kupokea kipigo cha mabao 3-2 dhidi ya Misri katika mchezo wa robo fainali uliochezwa kwenye Uwanja wa Adrar.
Misri Yatinga Nusu Fainali Baada, Ushindi wa 3-2 Vs Ivory Coast
Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa, Misri The Pharaohs walionesha uzoefu na uimara, wakifanikiwa kupindua meza dhidi ya mabingwa watetezi na kujihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo makubwa barani Afrika.
Muhtasari wa Mchezo: Misri 3-2 Ivory Coast
Misri walitangulia kupata bao la mapema dakika ya 3 kupitia Omar Marmoush, kabla ya Rami Rabia kuongeza bao la pili dakika ya 32. Dakika ya 40, Ivory Coast walipata bao kupitia goli la kujifunga la Fatouh, lililowapa matumaini kabla ya mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi, ambapo nahodha Mohamed Salah aliifungia Misri bao la tatu dakika ya 54. Ivory Coast walijaribu kurejea mchezoni baada ya bao la pili lililofungwa na Doue dakika ya 73, hata hivyo juhudi zao hazikutosha kuzuia ushindi wa Misri hadi filimbi ya mwisho.

Misri Yatinga Nusu Fainali AFCON 2025
Kwa ushindi huo, Misri wamefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali, ambapo watakutana na Simba wa Teranga, Senegal. Mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali kutokana na historia na ubora wa timu zote mbili katika soka la Afrika/Misri Yatinga Nusu Fainali Baada, Ushindi wa 3-2 Vs Ivory Coast.
Ratiba Rasmi ya Nusu Fainali AFCON 2025
Januari 14, 2026
- 20:00 β Senegal πΈπ³ vs πͺπ¬ Misri
- 23:00 β Nigeria π³π¬ vs π²π¦ Morocco
CHECK ALSO:






Weka maoni yako