Mitihani ya Kidato cha Sita na Ualimu Kuanza Mei 5, 2025: Mitihani ya Taifa ya kidato cha sita na ualimu itaanza tarehe 5 Mei, 2025, Tanzania Bara na Zanzibar.
Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza rasmi kuanza kwa Mitihani ya Taifa ya Kidato cha Sita (ACSEE), pamoja na Mitihani ya Cheti cha Ualimu na Stashahada, kuanzia kesho Mei 5, 2025, kwa Tanzania Bara na Zanzibar.
Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa NECTA Dk.Said Mohamed, jumla ya watahiniwa 145,285 wamejiandikisha kufanya mitihani kwa mwaka huu wa masomo 2025. Kati ya hao, watahiniwa 134,390 ni wa Kidato cha Sita, huku watahiniwa wa Mitihani ya Ualimu wakiwa 10,895.
Mitihani ya Kidato cha Sita na Ualimu Kuanza Mei 5, 2025
Watahiniwa wa Kidato cha Sita: 134,390
Watahiniwa wa Shule: 126,957
Watahiniwa wa Kujitegemea: 7,433
Watahiniwa wa Ualimu: 10,895
Ngazi ya Stashahada: 3,100
Wanaume: 1,751 (56.48%)
Wanawake: 1,349 (43.52%)
Ngazi ya Cheti: 7,795
Vituo vya Mitihani:
Mitihani ya Kidato cha Sita:
Shule za Sekondari: 982
Vituo vya Kujitegemea: 245
Mitihani ya Ualimu:
Vyuo vya Ualimu: 68
Kwa mujibu wa ratiba ya NECTA, mitihani ya Mafunzo ya Ualimu itafungwa Mei 19, 2025, huku mitihani ya kidato cha sita ikipangwa kufungwa rasmi Mei 26, 2025.
NECTA imewataka watahiniwa wote kufuata kwa makini miongozo ya mitihani ikiwa ni pamoja na kuzingatia ratiba rasmi, kuepuka udanganyifu na kuhakikisha wanatambua vituo vyao vya mtihani mapema.
Dk. Mohamed pia alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya shule, vyuo na mamlaka za mitihani ili kuhakikisha usalama, uthabiti na ufanisi katika kipindi chote cha mitihani.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako