Mkataba na Mshahara wa Moussa Balla Conté Yanga: Klabu ya Young African Sports Club (Yanga SC) imetangaza rasmi kumsajili kiungo mpya raia wa Guinea Moussa Balla Conté ambaye amewasili rasmi jangwani akitokea klabu ya CS Sfaxien ya Tunisia.
Usajili huo unatokana na vigezo vya kitaalamu na kifedha, hivyo kuakisi dhamira ya klabu hiyo katika kuimarisha orodha yake ya wachezaji mahiri kutoka Afrika.
Mkataba na Mshahara wa Moussa Balla Conté Yanga
Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vya ndani vya klabu hiyo, mkataba wa Conté unajumuisha mambo yafuatayo:
Moussa Balla Conté:
• Mkataba wa miaka 3 (Julai 2025 – Juni 2028)
• Mshahara wa $12K sawa na 31,239,619 Tsh (msimu wa kwanza), $13K sawa na 33,875,231 Tsh (wa pili), $14K sawa na 36,481,018 Tsh (msimu wa 3)
• Ada ya usaili ya $180K(468,594,289): Italipwa kwa awamu mbili – $60K (156,347,220) sasa, $60K (156,347,220) mnamo Agosti 2026 na 2027
• $500-1,302,893 tsh/kodi ya makazi
• Tikiti 2 za ndege ya kawaida kwa kila msimu

Mkataba huu unathibitisha kuwa Yanga SC imewekeza fedha nyingi katika usajili wa mchezaji mwenye uwezo wa kubadilisha mchezo hasa katika safu ya ulinzi. Mshahara na marupurupu mengine yanaashiria kuwa klabu hiyo inaimarika kifedha na inalenga kuleta ushindani wa kweli katika soka la Afrika.
Kulingana na wachambuzi wa masuala ya michezo, uamuzi wa kumpa Conté kandarasi ya kiwango hiki ni ishara kwamba klabu hiyo inalenga kupata mafanikio makubwa katika mashindano ya CAF na kutetea ubingwa wake wa kitaifa.
CHECK ALSO:







huyo balla conte ni mzimu jaman