Mr Blue Azindua Blue Records na Kutangaza Nyimbo 22 Mpya

Mr Blue Azindua Blue Records na Kutangaza Nyimbo 22 Mpya | Baada ya kimya cha muda mrefu msanii Mr.Blue aliibuka na kuzungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza tangu aanze kazi yake miaka 22 iliyopita. Akizungumza leo Aprili 2, 2025 amefichua sababu za kukwepa mahojiano kwa muda mrefu na kusema kuwa safari yake ya muziki imekuwa na changamoto nyingi ambazo zimemfanya ashindwe kuongea hadharani.

Mr Blue Azindua Blue Records na Kutangaza Nyimbo 22 Mpya

Katika mkutano huo Mr. Blue alitangaza rasmi kuzindua studio yake mpya inayojulikana kwa jina la Blue Records. Zaidi ya hayo, ili kusherehekea miaka 22 katika muziki, amepanga kuachia nyimbo 22, nne kati ya hizo zimetoka rasmi leo, huku zingine zikitarajiwa katika hatua tofauti.

Safari ya Muziki na Mafanikio

Mbali na kutangaza miradi mipya, Mr.Blue aliweka wazi jinsi ambavyo amenufaika na safari yake ya muziki, huku akitaja tamasha la Chaka Tu Chaka kuwa moja ya mambo yaliyomsaidia kwa kiasi kikubwa, hata kumsaidia kujenga nyumba anayoishi kwa sasa.

Mr Blue Azindua Blue Records na Kutangaza Nyimbo 22 Mpya
Mr Blue Azindua Blue Records na Kutangaza Nyimbo 22 Mpya

Katika mazungumzo yake Mr.Blue pia aliwataja wasanii waliomlea kimuziki kuwa ni pamoja na Afande Sele, Juma Nature, Dully Sykes na TID huku akisema pia ameweza kuwalea wasanii wachanga akiwemo Diamond Platnumz na wengine watakaoshirikishwa kwenye nyimbo zake 22 mpya.

“Ninatimiza miaka 22 kwenye game, natoa nyimbo 22 na kutambulisha Blue Records studio yangu mpya. Tuna vipaji vipya tunavyovilea pale. Nimelelewa na kina Afande Sele, Juma Nature, Dully Sykes na TID na mimi pia nina wadogo zangu kama Diamond na wengine ambao watasikika kwenye hizi nyimbo 22,” alisema Mr Blue.

Kwa hatua hii mpya, mashabiki wa Mr. Blue wanaweza kutarajia muziki mzuri zaidi kutoka kwake na kuona vipaji vipya vikigunduliwa kupitia Blue Records/Mr Blue Azindua Blue Records na Kutangaza Nyimbo 22 Mpya.

ANGALIA PIA: