Mufti wa Tanzania Athibitisha Eid Al-Fitr Kuadhimishwa Jumatatu

Mufti wa Tanzania Athibitisha Eid Al-Fitr Kuadhimishwa Jumatatu, Machi 31, 2025: Mufti Mkuu na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir, ametangaza mwezi huo kuonekana katika maeneo kadhaa ya nchi na nchi jirani, hali iliyowafanya Waislamu wa nchi hiyo kusherehekea sikukuu ya Eid al-Fitr siku ya Jumatatu, Machi 31, 2025.

Mufti wa Tanzania Athibitisha Eid Al-Fitr Kuadhimishwa Jumatatu

Akitoa taarifa hiyo jijini Dar es Salaam, Mufti Zubeir alisema:

“Nawatangazia Waislamu wote kuwa mwezi umeandama na umeonekana na kushuhudiwa sehemu nyingi katika nchi yetu. Pia, umeonekana waziwazi Kenya, Pemba, na Arusha. Hivyo, nimeuthibitisha mwezi huo na kesho itakuwa Eid.”

Mufti wa Tanzania Athibitisha Eid Al-Fitr Kuadhimishwa Jumatatu
Mufti wa Tanzania Athibitisha Eid Al-Fitr Kuadhimishwa Jumatatu

Maandalizi ya Eid al-Fitr Eid al-Fitr ni siku muhimu kwa Waislamu baada ya kumaliza mfungo wa Ramadhani. Katika siku hii, Waislamu hufanya sala maalum ya Eid, husherehekea kwa furaha, hutoa michango, na kushiriki chakula na familia na jamii nzima.

Maeneo ya kuona mwezi mwandamo umeonekana na kuthibitishwa katika maeneo kadhaa ikiwemo:

✅ Kenya

✅ Pemba

✅ Arusha

Sehemu mbalimbali za Tanzania Kwa taarifa hii rasmi kutoka kwa Mufti wa Tanzania, Waislamu wote nchini wanajiandaa kusherehekea Eid el Fitri kesho. Eid Mubarak njema kwa Waislamu wote!

CHECK ALSO: