Mzize na Dube Wafikisha Magoli 11, Yanga Yashinda Dhidi ya Tabora United: Young Africans SC (Yanga SC) imepata ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Tabora United kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora, kulipa kisasi cha kufungwa kwa mzunguko wa kwanza kwenye Ligi Kuu ya NBC.
Katika mechi hiyo, washambuliaji wa Yanga SC, Clement Mzize na Prince Dube waliendelea kung’ara baada ya kufunga mabao 11 kwa pamoja kwenye ligi.
Mzize na Dube Wafikisha Magoli 11, Yanga Yashinda Dhidi ya Tabora United
Matokeo ya Mchezo: Tabora United 0-3 Yanga SC
⚽ 21′ Mwenda
⚽ 57′ Clement Mzize
⚽ 68′ Prince Dube
Kwa ushindi huu, Wananchi wameimarisha nafasi yao kileleni mwa NBC Premier League, wakiwa na pointi 61 baada ya mechi 23.
MSIMAMO WA NBC PREMIER LEAGUE BAADA YA MECHI HII
1️⃣ Yanga SC – Mechi 23 | Pointi 61
2️⃣ Simba SC – Mechi 23 | Pointi 57
3️⃣ Azam FC – Mechi 23 | Pointi 48
4️⃣ Singida Black Stars – Mechi 24 | Pointi 47
Matokeo Mengine ya Ligi Kuu Tanzania Bara
✅ Fountain Gate 0-3 Singida Black Stars
✅ Pamba Jiji FC 1-1 Namungo FC
✅ KMC FC 3-2 Tanzania Prisons
ANGALIA PIA:
Weka maoni yako