Nafasi za Ajira Jeshi la Polisi Tanzania 2025 Sifa, Tarehe Muhimu na Jinsi ya Kutuma Maombi

Nafasi za Ajira Jeshi la Polisi Tanzania 2025 Sifa, Tarehe Muhimu na Jinsi ya Kutuma Maombi | Jeshi la Polisi Tanzania limetangaza nafasi za kazi kwa vijana wa kitanzania wenye shahada za kwanza, stashahada, cheti na kidato cha sita na nne. Nafasi hizi ziko wazi kwa waombaji wenye sifa, kwa mujibu wa tangazo rasmi lililotolewa na Inspekta Jenerali wa Polisi Tanzania (IGP), Camilius Wambura, Machi 20, 2025.

Nafasi za Ajira Jeshi la Polisi Tanzania 2025 Sifa, Tarehe Muhimu na Jinsi ya Kutuma Maombi

Sifa za Waombaji

Waombaji wote wanapaswa kuwa sifa zifuatazo:

a) Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.
b) Wazazi wake wawe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.
c) Awe amehitimu kidato cha nne au sita kuanzia mwaka 2019 hadi 2024.
d) Kwa waombaji wa kidato cha nne na sita pamoja na wenye Astashahada wawe na umri kuanzia miaka 18 hadi 25.
e) Kwa waombaji wa kidato cha nne wawe na ufaulu wa daraja la kwanza mpaka la nne (Division I – IV). Kwa waombaji wenye ufaulu wa daraja la nne (Division IV) wawe na ufaulu wa alama (Points) 26 hadi 28.
f) Kwa waombaji wa kidato cha sita wawe na ufaulu wa daraja la kwanza mpaka la tatu (Division I – III).
g) Wahitimu wa Shahada na Stashahada wawe na umri kuanzia miaka 18 hadi 30.
h) Awe na urefu usiopungua futi tano na inchi nane (5’8”) kwa wanaume, na futi tano na inchi nne (5’4”) kwa wanawake.
i) Awe na kitambulisho cha taifa au namba ya utambulisho kutoka mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA).
j) Awe na uwezo wa kuongea lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha.
k) Awe na afya njema kimwili na kiakili iliyothibitishwa na daktari wa Serikali.
l) Awe hajaoa/kolewa au kuwa na mtoto/watoto.
m) Awe hajawahi kutumia dawa za kulevya za aina yoyote.
n) Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya taaluma ya Polisi.
o) Awe hajaajiriwa au hajawahi kuajiriwa na taasisi nyingine ya Serikali.
p) Awe tayari kufanya kazi za Polisi mahali popote Tanzania.
q) Awe tayari kujigharamia katika hatua zote za usaili endapo ataitwa kwenye usaili.
r) Asiwe na alama za kuchorwa mwilini (tattoo).
s) Asiwe na kumbukumbu za uhalifu.
t) Kwa waombaji wenye elimu ya kiwango cha Shahada (NTA level 8), Stashahada (NTA level 6) na Astashahada (NTA Level 5 au NVA Level 3) wanatakiwa wawe na fani zilizotajwa kwenye tangazo hili.

Kwa wahitimu wa kidato cha nne na sita:
✔️ Wenye ufaulu wa daraja la kwanza hadi la nne kwa kidato cha nne, ambapo daraja la nne ni kuanzia alama 26 hadi 28.
✔️ Wenye ufaulu wa daraja la kwanza hadi la tatu kwa kidato cha sita.

Nafasi za Ajira Jeshi la Polisi Tanzania 2025 Sifa, Tarehe Muhimu na Jinsi ya Kutuma Maombi
Nafasi za Ajira Jeshi la Polisi Tanzania 2025 Sifa, Tarehe Muhimu na Jinsi ya Kutuma Maombi

Fani Zinazohitajika

Kwa waombaji wa shahada, stashahada na astashahada, fani zinazohitajika zinajumuisha:

Tanzania Bara (Shahada)

  • Uhandisi wa Umeme, Uhandisi wa Mitambo, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT)
  • Udaktari wa Binadamu, Uuguzi, Tiba ya Radiolojia
  • Usimamizi wa Ardhi, Sheria, Uchunguzi wa Jinai na Usalama wa Mtandao
  • Sayansi ya Mifugo, Sayansi ya Mazingira, Uandishi wa Habari
  • Lugha za Kigeni: Kifaransa, Kireno, Kichina na Kiarabu

Zanzibar (Shahada)

  • Uhasibu na Fedha, Uhandisi wa Kiraia, Sayansi ya Kompyuta
  • Uandishi wa Habari na Utangazaji, Sheria, Tiba ya Binadamu
  • Uuguzi, Dawa za Binadamu, Ugavi na Manunuzi

Stashahada (Diploma) na Astashahada (Certificate)

  • Udaktari wa Kinywa, Sayansi ya Uchunguzi wa Jinai, Usanifu wa Picha na Video
  • Ufundi wa Magari, Uhandisi wa Umeme, Usanifu wa Majengo
  • Uuguzi na Ukunga, Uendeshaji wa Mitambo, Muziki na Sanaa za Maonyesho
  • Usanifu wa Mavazi, Ushonaji, Ufundi wa Mabomba na Ujenzi
Nafasi za Ajira Jeshi la Polisi Tanzania 2025 Sifa, Tarehe Muhimu na Jinsi ya Kutuma Maombi
Nafasi za Ajira Jeshi la Polisi Tanzania 2025 Sifa, Tarehe Muhimu na Jinsi ya Kutuma Maombi

Jinsi ya Kutuma Maombi

📌 Mwisho wa kutuma maombi: Aprili 4, 2025

Utaratibu wa kutuma Maombi

  1. Waombaji wote wanatakiwa waandike barua za maombi kwa wenyewe kwa mkono (Handwriting) bila kusahau namba za simu na watumie anuani ya Mkuu wa Jeshi la Polisi S.L.P 961 DODOMA. Barua hiyo iambatishwe kwenye maombi ikiwa kwenye mfumo wa ‘pdf’.

  2. Waombaji wote wafanye maombi yao kupitia mfumo wa Ajira wa Polisi (TANZANIA POLICE FORCE – RECRUITMENT PORTAL) unaopatikana kwenye kiunganishi (link) cha tovuti ya Jeshi la Polisi (https://ajira.tpf.go.tz). Maombi yatakayowasilishwa kwa njia ya posta, barua pepe (email) au kwa mkono hayatapokelewa.

  3. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 04/04/2025.

Jeshi la Polisi limeeleza kuwa waombaji lazima wawe tayari kufanya kazi popote nchini na kuhudhuria mafunzo ya taaluma ya polisi. Ajira hizi ni fursa muhimu kwa vijana wa Kitanzania wenye sifa stahiki. Waombaji wanahimizwa kukidhi mahitaji yote na kuwasilisha maombi yao kabla ya tarehe ya mwisho.

CHECK ALSO: