Nafasi za Polisi 2025 Tangazo la Ajira Jeshi la Polisi

Nafasi za Polisi 2025 Tangazo la Ajira Jeshi la Polisi | Nafasi za Ajira Jeshi la Polisi Tanzania 2025 Sifa, Tarehe Muhimu na Jinsi ya Kutuma Maombi. Jeshi la Polisi Tanzania limetangaza nafasi za kazi kwa vijana wa kitanzania wenye shahada za kwanza, stashahada, cheti na kidato cha sita na nne.

Nafasi za Polisi 2025 Tangazo la Ajira Jeshi la Polisi, Nafasi hizi ziko wazi kwa waombaji wenye sifa, kwa mujibu wa tangazo rasmi lililotolewa na Inspekta Jenerali wa Polisi Tanzania (IGP), Camilius Wambura, Machi 20, 2025.

Nafasi za Polisi 2025 Tangazo la Ajira Jeshi la Polisi

Sifa za Waombaji

Waombaji wote wanapaswa kuwa:

  1. Raia wa Tanzania kwa kuzaliwa, wazazi wake wawe raia wa kuzaliwa.
  2. Wenye umri wa miaka 18 hadi 25 kwa kidato cha nne, sita na astashahada; na miaka 18 hadi 30 kwa stashahada na shahada.
  3. Wenye urefu usiopungua futi 5’8″ kwa wanaume na 5’4″ kwa wanawake.
  4. Wenye afya njema kimwili na kiakili iliyothibitishwa na daktari wa Serikali.
  5. Wasiokuwa na alama za kuchora mwilini (tattoo) wala kumbukumbu za uhalifu.
  6. Wasiokuwa wameoa, kuolewa au kuwa na watoto.
  7. Wenye vitambulisho vya Taifa au namba za utambulisho kutoka NIDA.
  8. Wenye uwezo wa kuongea Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha.

Kwa wahitimu wa kidato cha nne na sita:
✔️ Wenye ufaulu wa daraja la kwanza hadi la nne kwa kidato cha nne, ambapo daraja la nne ni kuanzia alama 26 hadi 28.
✔️ Wenye ufaulu wa daraja la kwanza hadi la tatu kwa kidato cha sita.

Nafasi za Polisi 2025 Tangazo la Ajira Jeshi la Polisi
Nafasi za Polisi 2025 Tangazo la Ajira Jeshi la Polisi

Fani Zinazohitajika

Kwa waombaji wa shahada, stashahada na astashahada, fani zinazohitajika zinajumuisha:

Tanzania Bara (Shahada)

  • Uhandisi wa Umeme, Uhandisi wa Mitambo, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT)
  • Udaktari wa Binadamu, Uuguzi, Tiba ya Radiolojia
  • Usimamizi wa Ardhi, Sheria, Uchunguzi wa Jinai na Usalama wa Mtandao
  • Sayansi ya Mifugo, Sayansi ya Mazingira, Uandishi wa Habari
  • Lugha za Kigeni: Kifaransa, Kireno, Kichina na Kiarabu

Zanzibar (Shahada)

  • Uhasibu na Fedha, Uhandisi wa Kiraia, Sayansi ya Kompyuta
  • Uandishi wa Habari na Utangazaji, Sheria, Tiba ya Binadamu
  • Uuguzi, Dawa za Binadamu, Ugavi na Manunuzi

Stashahada (Diploma) na Astashahada (Certificate)

  • Udaktari wa Kinywa, Sayansi ya Uchunguzi wa Jinai, Usanifu wa Picha na Video
  • Ufundi wa Magari, Uhandisi wa Umeme, Usanifu wa Majengo
  • Uuguzi na Ukunga, Uendeshaji wa Mitambo, Muziki na Sanaa za Maonyesho
  • Usanifu wa Mavazi, Ushonaji, Ufundi wa Mabomba na Ujenzi
Nafasi za Polisi 2025 Tangazo la Ajira Jeshi la Polisi
Nafasi za Polisi 2025 Tangazo la Ajira Jeshi la Polisi

Jinsi ya Kutuma Maombi

📌 Mwisho wa kutuma maombi: Aprili 4, 2025

  1. Barua ya maombi iandikwe kwa mkono na iambatishwe katika mfumo wa PDF.
  2. Maombi yafanywe kupitia mfumo rasmi wa Ajira wa Jeshi la Polisi unaopatikana kwenye tovuti/Nafasi za Polisi 2025 Tangazo la Ajira Jeshi la Polisi: https://ajira.tpf.go.tz.
  3. Maombi kupitia barua pepe, posta au kupeleka kwa mkono hayatapokelewa.

Jeshi la Polisi limeeleza kuwa waombaji lazima wawe tayari kufanya kazi popote nchini na kuhudhuria mafunzo ya taaluma ya polisi. Ajira hizi ni fursa muhimu kwa vijana wa Kitanzania wenye sifa stahiki. Waombaji wanahimizwa kukidhi mahitaji yote na kuwasilisha maombi yao kabla ya tarehe ya mwisho.

CHECK ALSO: